Huyu ndiye binti mrembo atakayeolewa na Augustino Lyatonga Mrema

>Ndoa kufungwa Alhamisi ya wiki hii huko Kiraracha mkoani Kilimanjaro

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

MWANADADA ambaye anatajwa kuwa na urembo wa asili, Bi.Halima (pichani) ndiye chaguo la Mwenyekiti wa Chama cha TLP,Augustino Lyatonga Mrema ambaye anatarajiwa kumuoa wiki hii.
Chanzo cha karibu na binti huyo kimeidokeza DIRAMAKINI BLOG kuwa, uamuzi wa Mheshimiwa Mrema kutupa ndoano kwa binti huyo unachochewa na sifa za kipekee alizonazo.

"Ni binti mpole, mkarimu, mwenye upendo wa asili ambaye tunamfahamu toka huko nyuma, huyu anafaa kabisa kwenda kumpa faraja Mheshimiwa Mrema,"kimeeleza chanzo hicho huku kikikataa kuweka wazi kuhusu binti huyo ni mkazi wa wapi hapa nchini.

"Kuhusu ni mkazi wa wapi au anatoka kijiji gani, vuta subira, wiki hii wakati tunakwenda kula pilau utapata taarifa zote, ukipata nafasi fika kwa Mzee Mrema, utapata taarifa kwa kina,"kiliongeza chanzo hicho katika mahojiano na DIRAMAKINI BLOG.

Mwishoni mwa wiki Mheshimiwa Mrema alitangaza kufunga ndoa siku ya Machi 24, 2022 katika Parokia ya Uwomboni kijijini kwake Kiraracha mkoani Kilimanjaro.

Mrema mwenye umri wa miaka 77 ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Parole nchini anafunga ndoa hiyo mara baada ya kumpoteza mke wake Rose Mrema aliyefariki dunia mwaka jana.

Alisema amepata, binti mwenye umri mdogo mweupe ambaye ni chaguo lake na watafunga pingu za maisha baada ya kufuata taratibu zote za kikanisa pamoja na ulipaji wa mahari.

Pia alisema,kilichomsukuma kuoa ni kumpata msaidizi wa maisha yake kwani yeye ni mzee na anahitaji mtu wa karibu wa kumwangalia na kumsaidia kwa ukaribu huku akiishukuru familia yake kwa kumkubalia.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news