Kamati ya Bunge yaguswa na ufanisi wa TANROADS, yatoa maelekezo

*Yatakiwa kuendelea kumsimamia kwa ukaribu mkandarasi anayetekeleza mradi wa BRT Awamu ya Pili

NA MWANDISHI WETU

MWENYEKITI Kamati ya Kudumu ya Bunge Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC), Jerry Slaa amesema Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) wameendelea kufanya kazi kubwa kwa taifa na kusimamia kikamilifu ujenzi wa miundombinu, kwa sababu wamepewa dhamana kubwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Samia Suluhu Hassan ambayo inawapasa kufanya kazi kwa bidii.
Slaa ameyasema hayo wakati Kamati ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma, ikipokea taarifa ya mradi wa Usafiri wa Haraka wa Mabasi (BRT) Awamu ya Pili, ambao unasuasua kukamilika tofauti na muda wa ukamilishaji wa mradi huo.
Mwenyekiti Kamati ya Kuduma ya Bunge Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC), Jerry Slaa akiongozana na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Ujenzi), Ludovick Nduhiye, Mtendaji Mkuu wa TANROADS,Mhandisi Rogatus Mativila na Barakaeli Mmari Mhandisi wa Miradi ya BRT wakati kamati hiyo ilipokagua ujenzi wa mradi wa Usafiri wa Haraka wa Mabasi (BRT) Awamu ya Pili Kariakoo-Mbagala tarehe 26,2022 jijini Dar es Salaam.

Ameitaka TANROARDS kuendelea kumsimamia kwa ukamilifu mkandarasi anayejenga miundombinu ya barabara ya Usafiri wa Haraka Awamu ya Pili kutoka Gerezani hadi Mbagala ili kuhakikisha Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan inatekeleza azma yake ya kufanya kazi kwa kasi kubwa.

Amebainisha kwamba, mradi huo ni muhimu na ndio maana Rais Samia alitoa maagizo ya kutaka mradi kumalizika kwa haraka ili wananchi waweze kunufaika na huduma ya usafiri ya mradi huo, ambao kumalizika kwake utakuwa na faida kubwa.
Barakaeli Mmari Mhandisi wa Miradi ya BRT akitoa maelezo kwa, MhE. Jerry Slaa ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) katikati na wajumbe wake, wa tatu kutoka kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Ujenzi), Ludovick Nduhiye na wa pili kutoka kushoto ni Mtendaji Mkuu wa TANROADS, Mhandisi Rogatus Mativila.
Moja ya daraja linalojengwa eneo la BP ambapo magari yatapita juu na treni itapita chini katika barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam. 

”TANROADS mnafanya kazi nzuri, lakini mwenendo wa makandarasi sio mzuri, mnapaswa kumfuatilia kwa karibu ili amalize mradi huu kwa wakati na kwa ufanisi mkubwa. Kwa kuwa kuchelewa kwake kunasababisha sintofahamu kwa wananchi,”amesema Jerry Slaa.

Kwa upande wake, Mjumbe wa Kamati hiyo, Augustine Vuma, naye aliitaka TANROADS kuhakikisha wanawasimamia wakandarasi mbalimbali nchini na kuwachukulia hatua wale wanaochelewesha utekelezaji wa miradi mbalimbali.
 
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Ujenzi), Ludovick Nduhiye akimsikilia mmoja wa wajumbe wa kamati hiyo ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Temeke, Mhe.Doroth Kilave allipokuwa akiuliza swali.

Baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo. 

Katika mradi huo, kazi za ujenzi wa majengo ikiwemo karakana moja, vituo vikuu viwili na vituo mlisho vinne imeshakamilika toka Julai 31, 2021 na sasa sehemu hiyo iko katika muda wa uangalizi wa mwaka mmoja kama mkataba unavyotaka.

TANROADS imeshakaa na mkandarasi na kuzungumza naye, ambaye kuchelewa kwake kulitokana na matatizo ya Uviko-19, hivyo Machi 27, 2023 mradi huo utamalizika.
Mtendaji Mkuu wa TANROADS,Mhandisi Rogatus Mativila akiwasilisha taarifa ya ujenzi wa mradi huo kwa kamati.
Wakati huo huo, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Ujenzi), Ludovick Nduhiye, amesema ushauri wote ulitolewa na Bunge kupitia kwa kamati hiyo utafanyiwa kazi ikiwemo kuusimamia mradi huo na kumalizika kwa wakati.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news