Kamati ya Bunge yatoa agizo Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA)

*Washuhudia maboresho makubwa Bandari ya Tanga

NA HADIJA BAGASHA

KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) imeagiza Mamlaka ya Bandari (TPA) kuwapeleka wataalamu kwenye bandari zilizoendelea ili kuchukua ujuzi utakaosaidia bandari za Tanzania kujiendesha kibiashara huku ikiishauri serikali kuacha siasa katika miradi mbalimbali inayotekelezwa.
Awali akizungumza mara baada ya kufanya ziara ya ukuguzi wa miradi mikubwa miwili inayoendelea kutekelezwa ya kuongeza kina cha bahari na ujenzi wa gati katika Bandari ya Tanga, Mwenyekiti wa kamati hiyo, Naghenjwa Kaboyoka amesema ameridhishwa na hatua ya utekelezaji wa miradi hiyo inayo lenga kuongeza biashara na kuinua pato la Taifa.

"Kamati yetu ilikuja kuangalia mradi unaotekelezwa na bandari na Shirika la Bandari Tanzania,kamati hii imeridhishwa sana na kazi iliyofanywa,tumeangalia upanuzi wa lango la kuingilia meli na kugeuzia meli,na katika mradi mkubwa ndio imebeba mradi wote,tumeona kina kimeongezeka kutoka mita tatu hadi mita kumi na tatu na bado kuna akiba ya mita mbili,"amesema Kaboyoka.
Aidha, kamati hiyo pia ilipata nafasi ya kuangalia vifaa vipya vinavyotumika katika bandari hiyo na kuridhishwa na utendaji kazi wake.

"Kamati imeshuhudia ununuzi wa cranes na kuridhika na utendaji wa kazi katika Bandari ya Tanga,ni kazi inayovutia na kupendeza kupata vitendea kazi vikubwa ambayo itaongeza ufanisi wa bandari zetu,"alisema Mheshimiwa Kaboyoka.
"Pia kamati imeridhika na juhudi zilizofanywa pamoja na UVIKO-19 uliokuwepo, lakini bado kazi imeenda vizuri sana,na tunaamini kwa fedha iliyotengwa kazi hii itamalizika,na tunawapongeza Mamlaka ya Bandari,Mtendaji mkuu pamoja na timu yake yote kwa kazi nzuri iliyofanyika katika Bandari ya Tanga,"amesema Kaboyoka.
Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Japhet Hasunga amesema uboreshwaji wa Bandari ya Tanga utarahisisha usafirishaji wa shehena na mafuta kwenda mikoa ya Kaskazini na nchi jirani.

Awali akizungumza wakati akitoa taarifa ya Bandari ya Tanga, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania, Eric Hamis,ameeleza kuwa lengo la Bandari ya Tanga ni kutumika kwa mikoa yote ya Kaskazini na Nchi za Afrika Mashariki na Kati.

Alisema, pamoja na kwamba upanuzi huo bado unaendelea wameanza kupokea meli kubwa za mizigo inayokwenda nje ya nchi.
"Tunataka kuipromote Bandari ya Tanga kuhudumia masoko ya nchi zinazotuzunguka kama DR Congo,Uganda,Burundi na Rwanda na ni rahisi kijografia na hii itaifanya bandari hii kuwa na ufanisi zaidi,"alisema Hamis.

Katika ziara hiyo kamati hiyo imeonesha kuridhishwa na matumizi ya fedha kwenye mradi wa upanuzi wa Gati na uchimbaji wa kina cha bahari katika Bandari ya Tanga.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news