SNV yaunga mkono juhudi za usafi Zahanati ya Kitangili Shinyanga

>Yawezeshwa kichomea taka, chombo cha kubebea taka

NA KADAMA MALUNDE

SHIRIKA la Maendeleo la Uholanzi (SNV – Netherlands Development Organization) kupitia Mradi wa Usafi wa Mazingira (WASH SDG) kwa ufadhili wa Serikali ya Uholanzi limekabidhi Kichomea Taka (Incinerator) na Chombo maalumu cha kubebea taka za hospitali (Biomedical Waste Carrier) ‘Guta’ katika Zahanati ya Kitangili iliyopo katika Kata ya Kitangili Manispaa ya Shinyanga.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga, Jomaary Satura (wa nne kulia aliyevaa miwani) na wadau wa afya na mazingira wakiangalia Kichomea taka (Incinerator) iliyotolewa na Shirika la SNV kwa ajili ya Zahanati ya Kitangili Kata ya Kitangili Manispaa ya Shinyanga.
Muonekano wa sehemu ya kuchomea taka katika Zahanati ya Kitangili iliyopo kwenye Kata ya Kitangili Manispaa ya Shinyanga iliyotengenezwa na Shirika la SNV. (Picha na Malunde 1 blog).

Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo Machi 21,2022 kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga, Jomaary Satura, Meneja Mradi wa Usafi wa Mazingira wa Shirika la SNV,Bw.Olivier Germain amesema, Incinerator ina gharama ya shilingi Milioni 19.3, Guta shilingi Milioni 5.6, gharama za kutengeneza Guta shilingi Milioni 1 hivyo jumla ya fedha zilizotumika ni shilingi Milioni 25.

Amesema, SNV imeendelea kushirikiana na Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) kuboresha hali ya usafi wa Mazingira Shinyanga katika maeneo ya umma, shule na sekta ya afya.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga, Jomaary Satura akizungumza wakati Shirika la SNV likikabidhi Kichomea Taka (Incinerator) na Chombo maalumu cha kubebea taka za hospitali ‘Guta’ katika Zahanati ya Kitangili iliyopo kwenye Kata ya Kitangili Manispaa ya Shinyanga tarehe 21 Machi,2022. Kulia ni Mganga Mkuu wa Manispaa ya Shinyanga Dkt. Elisha Ndaki. Wa kwanza kulia ni Mhandisi wa SNV, Hezron Magambo akifuatiwa na Meneja Mradi wa Usafi wa Mazingira Mjini wa Shirika la SNV,Bw.Olivier Germain.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Jomaary Satura akizungumza wakati Shirika la SNV likikabidhi Kichomea Taka ‘Incinerator’ na Chombo maalumu cha kubebea taka za hospitali ‘Guta’ katika Zahanati ya Kitangili iliyopo kwenye kata ya Kitangili Manispaa ya Shinyanga. Wa pili kushoto ni Diwani wa Kata ya Kitangili Mhe. Mariam Nyangaka akifuatiwa na Meneja Mradi wa Usafi wa Mazingira Mjini wa Shirika la SNV,Bw.Olivier Germain.
Meneja Mradi wa Usafi wa Mazingira Mjini wa Shirika la SNV,Bw. Olivier Germain akizungumza wakati Shirika la SNV likikabidhi Kichomea Taka ‘Incinerator’ na Chombo maalumu cha kubebea taka za hospitali ‘Guta’ katika Zahanati ya Kitangili iliyopo kwenye kata ya Kitangili Manispaa ya Shinyanga.

“Tunaushukuru uongozi wa Mkoa wa Shinyanga kwa ushirikiano ambao mmekuwa mkitupatia katika kutekeleza Mradi wetu wa Usafi wa mazingira. Tunaamini katika Incinerator hii itasaidia katika utunzaji wa mazingira katika zahanati ya Kitangili na Guta hili litasaidia katika ubebaji wa taka za hospitali na kuzileta hapa kwenye Incinerator kwa ajili ya kuziteketeza,”amesema Germain.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga, Mhe. Jomaary Satura amewashukuru SNV kwa msaada huo akibainisha kuwa Kichomea taka hicho kinaiongezea thamani Manispaa ya Shinyanga katika masuala afya na usafi wa mazingira.
Meneja Mradi wa Usafi wa Mazingira Mjini wa Shirika la SNV,Bw.Olivier Germain akizungumza wakati Shirika la SNV likikabidhi Kichomea Taka ‘Incinerator’ na Chombo maalumu cha kubebea taka za hospitali ‘Guta’ katika Zahanati ya Kitangili iliyopo kwenye Kata ya Kitangili Manispaa ya Shinyanga.
Meneja Mradi wa Usafi wa Mazingira Mjini wa Shirika la SNV,Bw.Olivier Germain akizungumza wakati Shirika la SNV likikabidhi Kichomea Taka ‘Incinerator’ na Chombo maalumu cha kubebea taka za hospitali ‘Guta’ katika Zahanati ya Kitangili iliyopo kwenye kata ya Kitangili Manispaa ya Shinyanga.
Meneja Mradi wa Usafi wa Mazingira Mjini wa Shirika la SNV,Bw. Olivier Germain (wa pili kulia) na Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Jomaary Satura (wa pili kulia) wakikata utepe wakati Shirika la SNV likikabidhi Kichomea Taka ‘Incinerator’ na Chombo maalumu cha kubebea taka za hospitali ‘Guta’ katika Zahanati ya Kitangili iliyopo kwenye Kata ya Kitangili Manispaa ya Shinyanga.
Meneja Mradi wa Usafi wa Mazingira Mjini wa Shirika la SNV,Bw. Olivier Germain (wa pili kulia) na Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Jomaary Satura (wa pili kulia) wakikata utepe wakati Shirika la SNV likikabidhi Kichomea Taka ‘Incinerator’ na Chombo maalumu cha kubebea taka za hospitali ‘Guta’ katika Zahanati ya Kitangili iliyopo kwenye kata ya Kitangili Manispaa ya Shinyanga.
“SNV wamekuwa wadau wakubwa katika masuala ya afya na mazingira ndani ya Manispaa yetu ya Shinyanga. Hii Tanzania ni kubwa lakini wao wametuchagua sisi Manispaa ya Shinyanga.Kama mna nafasi nyingine tunawaomba muendelee kuleta miradi mingine hapa, karibuni sana muendelee kuwekeza. Tunataka kuona Shinyanga inaendelea kuwa bora,”amesema Satura.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news