Kamati ya Siasa mkoani Singida yaendelea kukagua miradi ya maendeleo

NA MWANDISHI MAALUM

KAMATI ya Siasa Mkoa wa Singida imeendelea na ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo huku ikitoa rai kwa wananchi kujitokeza na kushiriki kikamilifu katika kazi za maendeleo.
Kauli hiyo imetolewa Machi 17, 2022 na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida, Alhaji Juma Kilimba wakati wa ziara ya Kamati ya Siasa Mkoa, inayoendelea kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani Singida. 

Alhaji Juma Kilimba amewaeleza wananchi wa Kijiji cha Mwasutianga katika Kata ya Irisya wilayani Ikungi kuwa, miradi yote inayotekelezwa mkoani Singida ni yao.

"Na hii miradi si ya viongozi, kwa hiyo hamna budi kushirikiana na Serikali ili kazi ziendelee kufanyika kwa haraka na kwa ufanisi,"amesema.

Wito huo ameutoa baada ya kuwakuta wananchi wakiendelea kufanya kazi katika Mradi wa Kituo cha Afya kinachojengwa Irisya ambapo kinatarajiwa kikikamilika kitaweza kuhudumia wakazi 30,000 katika maeneo hayo.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Binilith Mahenge amepongeza Kamati ya Siasa kwa kupitia kwa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida, Alhaji Juma Kilimba kwa kusema anafarijika anapoona kamati zikiendelea kufika katika miradi mbalimbali mkoani Singida.

Amesema kuwa, amejiridhisha na ujenzi unaoendelea katika Kituo cha Afya Irisya kwa kuona utendaji kazi unaendelea na kuona watu wengi wanaojitokeza kufanya kazi na usimamizi unaoendelea katika mradi huo.
Majengo ya Shule ya Msingi Kintandaa.
Mkurugenzi na Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Ikungi.

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Singida, Dkt.Denisi Nyiraha (wa pili kutoka kushoto) na Katibu wa UVCCM Mkoa, Bi.Vaileth Soka. Ziara hiyo inaendelea leo Machi 18, 2022 katika Manispaa ya Singida na Kikosi kingine kitaelekea katika Halmashauri ya Singida (DC).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news