Mbunge Regina Ndege aelekeza kero tatu muhimu za Manyara kwa Makamu wa Rais

*Ni kuhusu kituo cha afya, umeme na suala la shule moja ya bweni ya wasichana katika kila mkoa 

NA MARY MARGWE

MBUNGE wa Viti wa Maalum mkoani Manyara, Regina Ndege ameelekeza kero tatu kwa Makamu wa Rais, Dkt.Philip Mpango ikiwa ni pamoja na kuwepo kwa kituo cha afya Magara kisichokua na dawa pamoja na wahudumu wa afya, na hivyo kupelekea akina mama kufuata huduma ya kujifumgulia mbali na eneo hilo.
Akiongea juzi wakati wa ziara ya Makamu wa Rais, Dkt.Philip Mpango wakati akifungua daraja la Magara, Mbunge Regina Ndege alisema ameelekeza changamoto tatu ya kituo cha afya, umeme na suala la shule moja ya bweni ya wasichana katika kila mkoa, ambapo akianzia katika kituo hiko vha afya, alisema kilijengwa na wananchi kwa kushirikiana na serikali huku kikiwa kinafanya kazi isipokuwa hakina dawa huku wakiomba kuongezewa wahudumu wa afya..
Mheshimiwa Ndege alisema, Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan hakuna tena mwanamke kupata shida ya kutembea umbali mrefu kufuatia huduma ya afya, hivyo amemuomba Makamu wa Rais Dkt.Philip Mpango kuhakikisha changamoto hiyo inatafutiwa ufumbuzi wa haraka ili akina mama hao waweze kupata huduma stahili katika eneo husika.

Aidha, Ndege anaipongeza Serikali ya Awamu ya Sita kwa kazi nzuri inazoendelea kutekelezwa ikiwa ni pamoja na kujenga miundombinu mbalimbali kama shule, madarasa, pamoja na vituo vya afya.
"Akina mama inawalazimu wanapata tabu wakati wa kujifungua kuifuata huduma ya afya mbali na maeneo haya, kiasi kwamba wengine wapo ambao wanapoteza maisha, lakini watoto wadogo pia wanapata shida, kuna changamoto kubwa ya usafiri kwa maeneo haya kulingana na barabara tulizonazo.

"Kupitia ujio wako huu, tunakuomba Mheshimiwa Makamu wa Rais wewe ni msikivu, ni mpole ni mpenda watu, tunakuomba serikali yako isikie kilio cha eneo hili la hapa, wananchi hawa wapate huduma, madawa yawepo na madaktari waongezwe ili waweze kupata huduma hii kiurahisi zaidi,"aliongeza Mbunge huyo.

Aidha, pia aliipongeza serikali hiyo kwa kuanzisha mpango wa kuwa na umeme katika kila kaya, licha ya kuwa maeneo mengi umeme umefika, lakini bado vijiji vingine vingi havijapata umeme, isipokua yapo maeneo ambayo wananchi wanapata gharama kubwa ya kuingiza umeme badala ya ile ya sh.27,000 yapo maeneo wanaingiza umeme kwa sh.320,000.
Kufuatia hilo ameiomba serikali iweze kuisaidia wananchi hao kuhakikisha wanabaki kwenye kile kiasi cha sh.27,000 ambapo wananchi hao wanao uwezo wa kuuza kuku watatu ama wanne tayari watakua wamepata pesa na kuingiza umeme.

Mbali na hilo Mbunge huyo pia ameiomba serikali hiyo kupewa kipaumbele cha kupatiwa shule ya sekondari ya bweni kama ambavyo mkoa huo uko katika mpango huo, hivyo ameomba mkoa huo katika bajeti hiyo ya serikali kupata kipaumbele ili shule hiyo iweze kujengwa katika mpango huo wa mwaka huu.

"Nashukuru serikali yetu ya Awamu ya Sita kwa kuanzisha mpango wa kuwa na shule moja katika mkoa ya bweni ya wasichana, na mkoa wetu uko katika mpango huo wa kupewa shule, lakini kwa kupitia ujio wako huu niendelee kuiomba serikali kwamba kwa kuwa mkoa wetu uko katika ule mpango tunaomba tupewe kipaumbele, kwa sababu jografia ya mkoa huu Mheshimiwa Makamu wa Rais ni ngumu mno,"alisema Ndege.

Aidha aliongeza kuwa, "watoto wetu wa kike wa ni wachache wanaofanikiwa kwenda form five na six, na ni wachache wanaoweza kufika kwenye masomo ya sanyansi kwa sababu wengi wanaishia katika elimu ya ya form four, kwa hiyo kupitia ujio wako tunakuomba Mheshimiwa Makamu wa Rais kwa bajeti hii ya serikali Mkoa wetu wa Manyara tupewe kipaumbele ili shule hii ianze kujemgwa kwenye mpango huu wa mwaka huu,"aliongeza Mbunge.
"Kwa niaba ya akina mama wa mkoa wa Manyara, lakini kwa wananchi wa mkoa wa Manyara sisi tuseme kwamba asanteni sana Serikali ya Awamu ya Sita, kiukweli tumefarijika mno kama walivyotangulia kusema kaka zangu wa majimbo barabara hii ilikua ni changamoto kubwa, lakini kwa namna ambavyo serikali imefanya kazi kubwa, wananchi hawa wamefarijika sana na wana matumaini makubwa sana na serikali yetu ya awamu ya sita, tunaomba utifikishie salamu zetu kwa Mheshimiwa Mama Samia Suluhu Hassan kwamba sisi wananchi wa Manyara hatuna cha kumlipa zaidi ya kumuombea yeye na serikali yake aendelee kufanya kazi, asirudi nyuma, asonge mbele,"aliongeza Regina Ndege.
Hata hivyo, alisema mkoa huo uko vizuri ki chama na hivyo wataendelea kusonga mbele katika kuiunga mkono Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news