Mheshimiwa Mwakibete asisitiza usawa Sekta ya Uchukuzi

NA MWANDISHI MAALUM

NAIBU Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Uchukuzi), Atupele Mwakibete, amelitaka Baraza la Wafanyakazi la Sekta hiyo kutafuta suluhu ya changamoto za wafanyakazi na kuweka usawa ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa weledi.
Mwakibete amesema hayo jijini Dodoma wakati akifungua Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi lililowakutanisha kwa ajili ya kujadili masuala ya wafanyakazi na kupitia mpango wa Bajeti kwa kipindi cha mwaka 2022/2023.
Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Uchukuzi), Atupele Mwakibete, akizungumza na wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Sekta ya Uchukuzi (hawapo pichani), wakati akifungua baraza hilo katika ukumbi wa Mabele, Jijini Dodoma.

“Hakikisheni mnashughulikia malalamiko ya watumishi sehemu mnazozisimamia ili kuweka usawa na utendaji kazi mzuri kwa watumishi ikiwa ni pamoja na kupewa nafasi za kujiendeleza kielimu,”amesema Mwakibete.
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, (Sekta ya Uchukuzi), Bw Gabriel Migire akisisitiza Jambo kwa Baadhi ya wajumbe wa baraza la Wafanyakazi Sekta ya uchukuzi (hawapo pichani), wakati wa ufunguzi wa baraza hilo lilifanyika katika ukumbi wa Mabele jijini Dodoma.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Uchukuzi), Gabriel Migire, amemueleza Naibu Waziri huyo kuwa kwa sasa Sekta inafanya uhakiki na uchambuzi wa madeni ya watumishi hususan wastaafu na kuweka mikakati thabiti ya kulipa madeni hayo.
Baadhi ya Wajumbe wa Baraza la Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Uchukuzi), wakimsikiliza mgeni rasmi Naibu Waziri wa Wizara hiyo anayesimamia Sekta ya Uchukuzi, Atupele Mwakibete (hayupo pichani) wakati wa akifungua baraza hilo lililofanyika katika ukumbi wa Mabele jijini Dodoma.

“Baraza hili linakutana hapa kwa ajili ya kupitia utekelezaji wa mpango na Bajeti ya Sekta ya Uchukuzi kwa mwaka 2020/2021 ikiwa ni pamoja na masuala mbalimbali yanayowahusu watumishi,”amefafanua Migire.

Baraza la Wafanyakazi la Sekta ya Uchukuzi limeshirikisha Wajumbe wa Baraza ambao ni wakuu wa Idara na Vitengo, wakuu wa taasisi zote zilizoko chini ya Sekta hiyo pamoja na viongozi wa chama cha wafanyakazi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news