Rais Samia apokea ripoti na kutoa maelekezo

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

KIKOSI kazi cha kilichoteuliwa na Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi kimependekeza mchakato wa kupata Katiba Mpya uanze baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025, huku Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akikiagiza kulifanyia kazi na kupeleka mapendekezo.
Mwenyekiti wa kikosi kazi hicho, kinachojumuisha wajumbe 25 kutoka maeneo mbalimbali ikiwemo wanasiasa, asasi za kiraia, wanazuoni na wadau wa kamati za ulinzi na usalama, Profesa Rwekaza Mukandara ameeleza hayo leo Machi 21,22 Ikulu jijini Dar es Salaam.

Profesa Mukandara ametoa mapendekezo wakati akiwasilisha taarifa ya awali ya utendaji kazi wa kikosi hicho kwa Rais Samia Suluhu Hassan.

Kazi kubwa ya kikosi kazi hicho ni jukumu la kuangalia na kuchambua mwenendo wa hali ya demokrasia na namna ya kutatua changamoto zinazoikumba baadhi ya vyama vya siasa, ikiwemo mikutano ya hadhara.
ais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea Taarifa ya Kikosi Kazi cha kuratibu Maoni ya Wadau wa Demokrasia ya Vyama vingi vya Siasa kutoka kwa Mwenyekiti wa Kikosi Kazi hicho Profesa Rwekaza Mukandala Ikulu Jijini Dar es Salaam. (Picha na Ikulu).

Aidha, katika maelezo yake, Profesa Mukandara amesema, sababu za kutoa pendekezo hilo ni pamoja na kutoa fursa ya kuanisha dira mpya ya maendeleo ya miaka ijayo, itakayotoa mwelekeo wa katiba mpya.

“Pia kuna suala la kukosekana kwa muda wa kutosha kuanza kutumia Katiba mpya ndani ya kalenda ya uchaguzi 2025. Kuna haja ya kutoa fursa ya kufanya marekebisho ya sheria ya uchaguzi na kanuni zake. Jambo jingine ni kuna haja ya kutoa fursa ya kutosha ya kufanyia kazi masuala ya muda wa kati ikiwa ni pamoja na kuanisha masuala ya dira ya maendeleo,” amesema Profesa Mukandara.

Akizungumza baada ya kupokea taarifa hiyo, Rais Samia amesema kuwa, “Hili la Katiba mpya mtakwenda kulifanyia kazi na mtaleta mapendekezo yatakayotangazwa Watanzania wote wayaelewe.

"Mimi nakubaliana kuwa ni jambo la muda mrefu, lakini Watanzania wote waelewe. Lakini kwanza tukayafanyie kazi haya marekebisho tuliyoyasema haya kipindi hiki cha muda wa kati halafu huko mbele tuone je tuna haja ya kurekebisha katiba yetu pengine kutakuwa na haja sio ya kuandika mpya.

"Kurekebisha baadhi ya maeneo na hata kama tunaandika mpya lakini kazi kubwa inakuwa imefanyika kwenye marekebisho ambayo tunakuwa tumeyafanya kule ni kwenda kuingiza tuu kwenye hiyo katiba,”amesema.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news