Rais Samia asema Serikali imedhamiria kuimarisha mazingira ya kufundishia, kujifunza

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema Serikali inafanya jitihada za kuweka mazingira rafiki ya kufundishia na kujifunzia ili kila Mtanzania anufaike na fursa za elimu kwa manufaa yake binafsi na taifa kwa ujumla.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Benjamin Mkapa, Emanuel Mzena mara baada ya kuwasili Shuleni hapo leo Machi 7, 2022 kwa ajili ya kuzungumza na Wanafunzi wa Shule hiyo. (Picha zote na Ikulu).

Rais Samia amesema hayo wakati alipotembelea Shule ya Sekondari ya Benjamin Mkapa na kuzungumza na wanafunzi wa shule hiyo, iliyopo Ilala jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi mbalimbali pamoja Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Benjamin Mkapa, Wanafunzi wa Shule ya uhuru Mchanganyiko na Uhuru Msingi zilizopo eneo la Gerezani Ilala Jijini Dar es Salaam leo Machi 7, 2022.

Mhe. Rais Samia pia amesema Serikali imeendelea na Mkakati wa Kitaifa wa Elimu Jumuishi wa mwaka 2021/2022 hadi 2025/ 2026 ambao utazingatia utoaji elimu jumuishikatika ngazi zote za elimu ili kuwanufaisha pia wanafunzi wenye mahitaji maalumu.

Pamoja na kujenga shule na madarasa ya wanafunzi wenye mahitaji maalum na jumuishi, Serikali imeshatumia zaidi ya shilingi bilioni 5.9 kununua vifaa kwa ajili ya wanafunzi hao katika elimu ya msingi, sekondari na vyuo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akigawa vifaa mbalimbali vya michezo kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari Benjamini Mkapa, Shule ya Msingi Uhuru pamoja na Shule ya Uhuru Mchanganyiko leo Machi 7, 2022.
Sehemu ya Viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Dar es Salaam, wanafunzi wa Shule ya Sekondari Benjamini Mkapa, baadhi ya Wanafunzi wa Shule ya Msingi Uhuru mchanganyiko wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan wakati alipokuwa akiwahutubia leo Machi 7, 2022.
Mbali na hapo, Serikali imetoa mafunzo ya aina tofauti kwa walimu 3980 wenye taalumaya Elimu Maalum katika ngazi ya Msingi, Sekondari na Ualimu.

Mafunzo hayo yametolewa kwa wadhibiti ubora ili waweze kukagua madarasa maalum na jumuishi pamoja na miundombinu kwa ajili ya wanafunzi wenye mahitaji maalum.
Wakati huo huo, Serikali ilifanya ubainishaji wa watoto wenye mahitaji maalum ambao wamefikisha umri wa kuanza shule na kubaini watoto 28,698 wenye mahitaji maalum kati ya 59,784 waliochunguzwa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news