RC Kafulila:Tukubaliane wanawake wana uwezo mkubwa uliofichika,tuutambue na kuutumia

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

MKUU wa Mkoa wa Simiyu, Mheshimiwa David Kafulila amesema kuwa, wanawake ni jeshi kubwa ambalo Mungu amelikiria vipawa vya kipekee katika uongozi.
Kafulila ameyabainisha hayo leo Machi 8, 2022 katika kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani ambayo kimkoa yamefanyika wilayani Itilima.

"Lazima tukubaliane wanawake wana uwezo mkubwa uliofichika na hivyo tuutambue na kuutumia. Nimesoma ripoti ya WOMEN COUNT 2020 inaonesha kwamba kati ya kampuni kubwa kabisa 350 ndani ya soko kubwa la mitaji duniani la London Stock Exchange, ni kampuni 14 tu zinazongozwa na wanawake .

"Hata hivyo, kampuni zenye zaidi ya theluthi moja kwenye uongozi zilionekana kutengeneza faida mara 10 ya kampuni zisio na wanawake kwenye uongozi,"amefafanua Mheshimiwa Kafulila. 

Kwa Tanzania maadhimisho hayao yameongozwa na kaulimbiu isemayo “Kizazi cha haki na usawa kwa maendeleo endelevu, tujitokeze kuhesabiwa”.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news