Serikali yatoa maelekezo muhimu Katoro kuhusu anuani za makazi

NA MWANDISHI MAALUM

NAIBU Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Kundo Mathew ameutaka uongozi wa Kata ya Katoro mkoani Geita kwenda kuzingatia sifa na vigezo kwa ajira zitakazotolewa ili kukamilisha zoezi la Anuani za Makazi.
Naibu Waziri Kundo ameyasema hayo katika Kata ya Katoro iliyopo Wilaya ya Geita Vijijini mkoani Geita wakati wa kikao kazi cha viongozi na watendaji wa kata hiyo kuhusu utekelezaji wa operesheni Anuani za Makazi.
Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Mhandisi Kundo Mathew (Mb) akizungumza wakati wa kikao kazi cha kuwajengea uelewa viongozi na watendaji kuhusu utekelezaji wa operesheni ya Anuani za Makazi kilichofanyika katika Kata ya Katoro iliyopo Wilaya ya Geita Vijijini mkoani Geita.

“Sitegemei kuona kwamba vijana ambao wanakwenda kupata ajira katika zoezi hili wanatoka Dar es Salaam, wanatoka Mwanza wala wanatoka Geita, natarajia kuona kwamba zoezi hili linakwenda kusimamiwa na wazawa na ajira hizi ziende zikanufaishe wananchi wa kata ambayo zoezi linafanyika,”amesema Mhandisi Kundo.

Aidha, Mhandisi Kundo amewaeleza kuwa pamoja na faida nyingine, mfumo huo utaiwezesha Serikali ya Mhe.Rais Samia kuleta maendeleo katika Kata ya Katoro kwa urahisi kwani idadi ya watu wanaoishi katika kata hiyo itakuwa inajulikana baada ya kushiriki kikamilifu katika maozezi hayo mawili ya anwani za makazi na lile la Sensa ya Watu na Makazi.
Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za Posta wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Caroline Kanuti (wa kwanza kushoto) akitoa maelekezo jinsi ya kupata Postikodi ya Kata kwa kutumia simu ya mkononi wakati wa kikao kazi cha kuwajengea uelewa Viongozi na Watendaji wa Kata ya Katoro iliyopo Wilaya ya Geita Vijijini mkoani Geita kuhusu utekelezaji wa operesheni Anuani za Makazi
Mkuu wa Wilaya ya Geita, Mhe. Wilson Shimo akizungumza wakati wa kikao kazi cha kuwajengea uelewa Viongozi na Watendaji wa Kata ya Katoro kuhusu utekelezaji wa operesheni Anuani za Makazi. Kikao kazi hicho kilifunguliwa na Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Mhandisi Kundo Mathew (Mb).
Meneja wa TCRA Kanda ya Ziwa, Mhandisi Francis Mihayo akizungumza na viongozi na watendaji wa Kata ya Katoro iliyopo Wilaya ya Geita Vijijini mkoani Geita kuhusu utekelezaji wa operesheni Anuani za Makazi. Kikao kazi hicho kilifunguliwa na Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Mhandisi Kundo Mathew(Mb).
Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za Posta wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Caroline Kanuti akizungumza wakati wa kikao kazi cha kuwajengea uelewa Viongozi na Watendaji wa kata ya Katoro iliyopo Wilaya ya Geita Vijijini Mkoani Geita kuhusu utekelezaji wa operesheni Anwani za Makazi. Kikao kazi hicho kilifunguliwa na Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Mhandisi Kundo Mathew (Mb).

Awali Mkuu wa Wilaya ya Geita, Wilson Shimo amesema wananchi wake tayari wanalifahamu vizuri jambo la anuani za makazi na ni matumaini yake kwamba kazi nzuri itakwenda kufanywa na wakazi hao wa Kata ya Katoro ili kuhakikisha na wao wanajumuishwa kikamilifu katika maendeleo yatakayoletwa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan.

Zoezi la utekelezaji mfumo wa Anuani za Makazi linatakiwa kukamilika mapema ifikapo mwezi Mei, 2022 ili kuwezesha zoezi lingine la Sensa ya Watu na Makazi likafanyike kwa urahisi mwezi Agosti, 2022.

Post a Comment

0 Comments