SIMBA PIGA BELKANE;Na kwa Mkapa hatoki

LEO wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya Kimataifa, Simba SC watachuana na RS Berkane ya Morocco katika mchezo wao wa nne wa hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho barani Afrika.
Berkane tayari wameshatua nchini kwa mchezo huo utakaopigwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar er Salaam. 

Dkt. Mohamed Omary Maguo ambaye ni Mshairi wa Kisasa na Mhadhiri na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Masoko Chuo Kikuu Huria cha Tanzania ana maneno yafuatayo;


1


Bekane hachomoki


Na kwa Mkapa hatoki


Simba ni kama bunduki


Bekane tabafuliwa



2


Ni simba yenye mikiki


Inang'ata kama nyuki


Nye' mashabiki lukuki


Tumwagike kwa Mkapa



3


Wana Simba ndakindaki


Twendeni tukale uki


Kandanda ja mishikaki


Simba watatupa raha


4


Simba yenye mikakati


Inakwenda na wakati


Mpira Safi natiki


Simba yetu Tanzania



Faharisi


Natiki=Tamthiliya


Uki=Asali



MTUNZI


Dkt. Mohamed Omary Maguo


Mshairi wa Kisasa


Mhadhiri na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Masoko


Chuo Kikuu Huria cha Tanzania


13/3/2022

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news