Tanzania, Ireland zaahidi makubwa zaidi kupitia uhusiano na ushirikiano

NA MWANDISHI MAALUM

SERIKALI ya Tanzania na Ireland zimeahidi kuendeleza uhusiano na ushirikiano uliopo baina ya nchi hizo kwa manuufaa ya pande zote mbili.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula akizungumza na Balozi wa Canada nchini Mhe. Pamela O’Donnell wakati wa sherehe za maadhimisho ya Siku ya Mtakatifu Patrick zilizofanyika nyumbani kwa Balozi wa Jamhuri ya Ireland nchini,Mary O’Neil (kulia) akiwaangalia.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula akizungumza wakati wa sherehe za maadhimisho ya Siku ya Mtakatifu Patrick zilizofanyika nyumbani kwa Balozi wa Jamhuri ya Ireland nchini.
Balozi wa Ireland nchini Mhe. Mary O’Neil akizungumza wakati wa sherehe za maadhimisho ya Siku ya Mtakatifu Patrick zilizofanyika nyumbani kwake jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula akiwa na Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki , Balozi Swahiba Mndeme (kulia) wakimsikiliza Balozi wa Ireland nchini Mhe. Mary O’Neil akizungumza wakati wa sherehe za maadhimisho ya Siku ya Mtakatifu Patrick zilizofanyika nyumbani kwake jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula (Mb) ametoa ahadi hiyo aliposhiriki katika maadhimisho ya Siku ya Mtakatifu Patrick ambayo huadhimishwa na Jamhuri ya Ireland tarehe 17 ya kila mwaka.

Akizungumza katika maadhimisho ya siku hiyo Waziri wa Mulamula ameishukuru Serikali ya Jamhuri ya Ireland kwa kuendelea kuwa mdau mkubwa wa maendeleo wa Tanzania hasa katika nyanja za kusaidia kaya masikini, elimu na kuwajengea uwezo wanawake na watoto wa kike nchini.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula akizungumza na Balozi wa Comoro na Mkuu wa Mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini, Mhe.Ahmada El Badaoui Mohamed Fakih wakati wa sherehe za maadhimisho ya Siku ya Mtakatifu Patrick zilizofanyika nyumbani kwa Balozi wa Ireland jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Kenya nchini, Mhe. Dan Kazungu (katikati) akijadili jambo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula (kulia) walipokutana nyumbani kwa Balozi wa Ireland nchini, Mhe. Mary O’Neil kwenye sherehe za maadhimisho ya Siku ya Mtakatifu Patrick ambayo huadhimishwa nchini humo tarehe 17 Machi ya kila mwaka.

Amesema, Serikali inathamini mchango wa Ireland kwa Tanzania na kusisitiza kuwa itaendeleza uhusiano na ushirikiano uliopo baina ya nchi hizo ili kufikia maendeleo ya kweli kwa pamoja.

Naye Balozi wa Ireland nchini Mhe. Mary O’Neil ameahidi kuendelea kuisaidia Tanzania katika jitihada za kuwaletea wananchi wake maendeleo.

Amepongeza ushirikiano uliopo kati ya Tanzania na Ireland na kuahidi kuendeleza ushirikiano huo kwa faida ya wananchi wa nchi zote.
Baadhi ya mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao Tanzania walioshiriki sherehe za maadhimisho ya Siku ya Mtakatifu Patrick zilizofanyika nyumbani kwa Balozi wa Jamhuri ya Ireland jijini Dar es Salaam.

Maadhimisho ya siku hiyo yamezinduliwa rasmi leo Machi 2, 2022 jijini Dar es Salaam katika makazi ya Balozi wa Ireland nchini na kuhudhuriwa na Mabalozi na Wawakilishi wa taasisi za Kimataifa wanaoziwakilisha nchi na Mashirika yao hapa nchini.

Siku ya Mtakatifu Patrick huadhimishwa kila ifikapo tarehe 17 Machi nchini Ireland kuadhimisha kuwasili kwa ukristo nchini humo na kusherehekea urithi wa utamaduni wa watu wa Ireland kwa ujumla.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news