Tanzania yazifikia fursa za Kimataifa kuhusu uboreshaji wa Sekta ya Elimu

*Prof.Mkenda ashiriki Mkutano wa Kimataifa wa Doha Forum

NA MWANDISHI MAALUM- WyEST

WAZIRI wa Elimu,Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda ameshiriki Mkutano wa Kimataifa Doha Forum kuhusu masuala ya Maendeleo uliofanyika Machi 26, 2022.
Prof. Adolf Mkenda, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia akiwa katika mazungumzo maalum na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Education Above All la Qatar Fahad Al- Sulaiti juu ya ushirikiano na Tanzania katika kuimarisha elimu Doha Qatar.

Mkutano huo unaofanyika kila mwaka umeshirikisha viongozi na wataalamu kutoka nchi mbalimbali Duniani ambapo Mwaka huu umelenga katika kujadili jinsi ya kuleta mabadiliko chanya katika maendeleo.

Moja ya ajenda katika mjadala wa mkutano huo ni mabadiliko halisi na chanya katika elimu hususa baada ya athari za UVIKO 19 ambapo Waziri wa Elimu ameshiriki katika majadiliano hayo ambayo yanahusisha mawaziri kutoka nchi tisa ikiwemo Qatar,Tanzania,Uganda, Sudan Kusini, Siera Leone na Somalia.
Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda akizungumza na Viongozi kutoka UNICEF walipokutana katika Mkutano wa Kimataifa wa Maendeleo DOHA FORUM unaofanyika jijini Doha, Qatar.

Akizungumza katika jukwaa hilo la majadiliano,  Prof. Mkenda amesema Tanzania kwa sasa iko katika hatua ya kufanya mapitio ya Sera na Mitala ili kuhakikisha Elimu inayotolewa inazingatia kujenga ujuzi na kwamba mpango huo ni shirikishi.

Naye Mtendaji Mkuu wa Shirika la Education Above all la Qatar, Mhe. Fahad Al-Sulaiti amesema wakati umefika wa mataifa kuleta Mabadiliko sahihi katika Elimu kwa kuwa na Mitaala Sahihi, mbinu za kisasa za kufundishia, matumuzi ya TEHAMA katika kufundisha na ujifunzaji kulingana na mipango endelevu ya Nchi na kusisitiza juu ya suala la kuongeza uwekezaji katika Sekta ya Elimu.
Prof Adolf Mkenda Waziri wa Elimu Sayansi an Teknolojia akiwa katika Picha na Baadhi ya Mawaziri waluohudhururia Jukwaa la majadiliano ya kuleta mabadiliko sahihi katika Elimu ylililofanyika sambamba na Mkutano wa Kimataifa wa Maendeleo Doha Forum jijini Doha, Qatar.

Wakati huo huo Waziri wa Elimu amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji huyo juu ya ushirikiano katika kuboresha Elimu Tanzania.

Post a Comment

0 Comments