Watanzania 274 tayari wamenufaika na programu za masomo ya muda mrefu nchini Japan, huku wanataaluma 16 wakielekea nchini humo kwa masomo ya uzamili na mafunzo ya vitendo katika kampuni za Kijapani.



Tanzania na Japan zimeendelea kuimarisha ushirikiano katika elimu, kupitia fursa zinazolenga kuongeza ujuzi na weledi wa watumishi na wataalamu wa Tanzania.
Hayo yamesemwa jijini Dar es Salaam na Mwakilishi wa JICA nchini Tanzania, Dk. Kuge Katsuya, wakati wa hafla ya kuwaaga wanataaluma hao 16.
Amesema programu hiyo ya ABE Initiative inawapa Watanzania nafasi ya kusoma fani mbalimbali, ikiwemo sera za umma, madini na uhandisi.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo

























