Utabiri wa hali ya hewa saa 24 zijazo, kuna matarajio ya radi, ngurumo na mvua

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

UTABIRI wa hali ya hewa leo unaletwa kwenu na mchambuzi, Tunza Sanane kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA). 

Kwa mujibu wa TMA, mikoa ya Morogoro (Kusini), Lindi, Ruvuma, Mtwara,Songwe, Iringa, Mbeya na Njombe kuna matarajio ya mawingu, mvua na ngurumo na vipindi vifupi vya jua.

Huku kwa upande wa Rukwa na Tabora kutakuwa na matarajio ya mvua na ngurumo na vipindi vya jua ambapo Kagera, Geita, Kigoma na Katavi kuna matarajio ya ngurumo na jua.
 
Mikoa ya Dodoma, Singida na Morogoro (Kaskazini) kuna matarajio ya mvua na vipindi vya jua. Huku visiwa vya Unguja na Pemba, Dar Es Salaam, Tanga, Arusha, Manyara, Kilimanjaro, Mwanza, Shinyanga, Simiyu, Mara, Pwani ikijumuisha visiwa vya Mafia matarajio ni jua.

UPEPO WA PWANI
 
Kwa mujibu wa TMA, upepo wa Pwani unatarajiwa kuvuma kwa kasi ya kilomita 30 kwa saa kwa Pwani yote kutoka KASKAZINI MASHARIKI kwa Pwani ya Kaskazini, na kutoka KASKAZINI MAGHARIBI kwa Pwani ya Kusini.

HALI YA BAHARI
 
Kwa upande wa bahari, TMA imebainisha kuwa, yanatarajiwa mawimbi makubwa kiasi. Utabiri huu wa saa 24, unaanza leo saa 3 usiku.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news