Utabiri wa hali ya hewa saa 24 zijazo/Weather forecast March 25th,2022 starting 21:00 tonight

*MVUA NA NGURUMO INATARAJIWA KATIKA BAADHI YA MAENEO YA MIKOA YA TABORA, KIGOMA, KATAVI, KAGERA, GEITA, MWANZA, SHINYANGA, SIMIYU NA MARA

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

UTABIRI wa hali ya hewa kwa 24 zijazo kuanzia 3:00 usiku leo Machi 25,2022 unaletwa na mchambuzi Amina Salehe kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA).
Mikoa ya Kigoma, Tabora, Katavi, Kagera, Geita, Mwanza, Mara, Simiyu na Shinyanga inatarajiwa kuwa mvua na ngurumo kwa maeneo machache na jua.

Aidha kwa upande wa mikoa ya Kilimanjaro na Arusha kuna matarajio ya mvua nyepesi na jua, huku Ruvuma, Lindi, Mtwara, visiwa vya Unguja na Pemba, Dodoma, Singida, Morogoro na Manyara, Tanga, Dar es Salaam, Pwani(ikijumuisha visiwa vya Mafia), Rukwa, Songwe, Mbeya, Iringa na Njombe matarajio yakiwa ni jua.

UPEPO WA PWANI: Unatarajiwa kuvuma kwa kasi ya kilomita 20 kwa saa kwa Pwani yote kutoka Kusini Mashariki kwa Pwani ya Kaskazini na kutoka Mashariki kwa Pwani ya Kusini.

HALI YA BAHARI: Mawimbi madogo.WEATHER FORECAST 25/03/2022:THUNDERSHOWERS IS EXPECTED OVER SOME AREAS OF TABORA, KIGOMA, KATAVI, KAGERA, GEITA, MWANZA, SHINYANGA, SIMIYU AND MARA REGIONS.
Weather forecast for the next 24 hour starting 21:00 tonight, by analyst Amina Salehe from Tanzania Meteorological Authority (TMA).

Post a Comment

0 Comments