Utabiri wa hali ya hewa Tanzania saa 24 zijazo...Weather forecast for the next 24 hours

UTABIRI wa hali ya hewa saa 24 zijazo kuanzia saa tatu usiku leo Machi 14,2022 unaletwa kwenu na mchambuzi, Amina Saleh kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA).
 
Kwa mujibu wa TMA, mikoa ya Ruvuma, Kagera, Geita, Kusini mwa Mkoa wa Morogoro, Kigoma, Katavi, Tabora, Rukwa, Songwe, Mbeya, Iringa na Njombe inatarajiwa kuwa na hali ya mawingu kiasi, mvua na ngurumo katika maeneo machache na vipindi vya jua.

Aidha, mikoa ya Dodoma na Singida inatarajiwa kuwa na hali ya mawingu kiasi, mvua katika maeneo machache na vipindi vya jua.

Mikoa ya Lindi na Mtwara inatarajiwa hali ya mawingu kiasi, mvua nyepesi katika maeneo machache na vipindi vya jua.

Visiwa vya Unguja na Pemba, Mikoa ya Dar es Salaam, Tanga, Kaskazini mwa Mkoa wa Morogoro, Arusha, Manyara, Kilimanjaro, Pwani (ikijumuisha Visiwa vya Mafia), Mwanza, Mara, Shinyanga na Simiyu inatarajiwa kuwa na hali ya mawingu kiasi na vipindi vya jua.

Upepo wa Pwani: Unatarajiwa kuvuma kwa kasi ya kilomita 30 kwa saa kwa Pwani yote kutoka Kaskazini Mashariki kwa Pwani ya Kaskazini na kutoka Kaskazini kwa Pwani ya Kusini.

Hali ya Bahari: Inatarajiwa kuwa na Mawimbi Makubwa kiasi huku matarajio kwa siku ya Jumatano tarehe 16/03/2022 huenda kukawa na mabadiliko kidogo.

WEATHER FORECAST FOR THE NEXT 24 HOURS
 
THUNDERSHOWERS ARE EXPECTED OVER GEITA, KAGERA, TABORA, KIGOMA, KATAVI, RUKWA, MBEYA, SONGWE, MOROGORO(KUSINI), IRINGA, NJOMBE AND RUVUMA REGIONS.
Weather forecast for the next 24 hours starting tonight at 9:00 p.m on 14/03/2022 as presented by weather analyst Amina Saleh from Tanzania Meteorological Authority (TMA).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news