Wanufaika mikopo Elimu ya Juu wajitokeza kulipa madeni yao

Afisa Mikopo Mwandamizi wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), Sophia Saidan akitoa huduma kwa wateja mbalimbali waliotembelea Banda la HESLB tarehe 13 Machi, 2022 mkoani Tanga wakati wa kampeni ya SIFURISHA inayoendelea katika Ofisi za Halmashauri ya Jiji la Tanga. Kampeni hiyo inalenga kuhumasisha urejeshaji wa mikopo ya elimu ya juu kutoka kwa wanufaika.Maafisa Mikopo wa HESLB wakitoa huduma mbalimbali kwa wateja mkoani Tanga wakati wa Kampeni ya SIFURISHA inayolenga kuhamasisha urejeshaji wa mikopo ya elimu ya juu inayoendelea katika Ofisi za Halmashauri ya Jiji la Tanga.
Meneja wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Ofisi ya Arusha, PatricK Shoo akimkabidhi barua ya kumaliza deni la Mkopo wa elimu ya juu shilingi milioni 11,345,845.20  mkoani Tanga, Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Wilaya ya Handeni, Mhe. Yusuph Abdallah wakati wa kampeni ya SIFURisha inayoendelea katika Ofisi ya Halmashauri ya Jiji la Tanga.
Afisa Mikopo Mwandamizi wa HESLB, Sunday Charles akimkabidhi barua ya kumaliza deni la mkopo wa elimu ya juu shilingi milioni 9,736,900.90, mtumishi wa Halmashauri ya Jiji la Tanga Mary Siphaelly mara ya baada kulipa kiasi cha shilingi milioni 1,888,000 na kumaliza deni la mkopo huo wakati wa kampeni ya SIFURISHA inayoendelea katika Ofisi za Halmashauri ya Jiji la Tanga.(PICHA NA HESLB).

Post a Comment

0 Comments