Wasichana wa Tanzania waiacha Botswana hoi kwa 4-0

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

TIMU ya taifa ya wasichana ya Tanzania chini ya umri wa miaka 17 (U17) imefanikiwa kwenda Raundi ya Tatu kufuzu Kombe la Dunia.
Ni baada ya ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya wenyeji, Botswana kupitia mtanange wa Machi 20,2022 uliopigwa katika dimba la Obeid Itan Chilume lililopo Francistown, Botswana.

Neema Kinega dakika ya 28 alianza kuwapa raha Watanzania na baadaye Clara Luvanga akatupia mabao matatu dakika za 62, 63 na 81.

Kutokana na matokeo hayo, Tanzania inafuzu kwa ushindi wa jumla ya mabao 11-0 kufuatia kuwachapa Botswana 8-0 kwenye mechi ya kwanza jijini Zanzibar.

Aidha, mtanage ujao unatarajiwa kupigwa kati ya Tanzania na Burundi kutafuta nafasi ya kuingia hatua ya mwisho ya mchujo wa kuwania tiketi ya India baadaye mwaka huu.
Watanzania wameonesha kuwa na furaha baada ya timu hiyo ya wasichana kuwapa heshima ya kipekee katika michuano ya Kimataifa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news