Watumishi wa umma fanyeni kazi kwa bidii, weledi-Waziri Balozi Dkt.Chana

NA MWANDISHI MAALUM

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Balozi, Dkt. Pindi Chana amewataka watumishi wa umma kufanya kazi kwa weledi, ufanisi na kuzingatia taratibu na kanuni zilizopo kwa mujibu wa sheria ili kutoa huduma bora kwa umma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Balozi. Dkt. Pindi Chana akizungumza wakati wa uzinduzi wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi hiyo katika Ukumbi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Machi 19, 2022 Jijini Dodoma.

Mhe. Pindi alitoa kauli hiyo Machi 19, 2022 katika Ukumbi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Njedengwa, Jijini Dodoma wakati akifungua kikao cha Baraza la Wafanyakazi la Ofisi hiyo na kupokea na kujadili taarifa ya utekelezaji wa bajeti ya Ofisi ya Waziri mkuu kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2021/2022 na makadirio ya bajeti mwaka 2022/ 2023 ambapo aliwahimiza kuwa wabunifu katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku na kuhudumia umma kama inavyokusudiwa na Serikali.

Alisema kwamba lengo la kuanzishwa kwa mabaraza ya wafanyakazi ni kuongeza ufanisi na tija katika sehemu za kazi, waajiri na wafanyakazi kubadilishana mawazo na kubaini mbinu mbalimbali za kukabiliana na changamoto zinazowakabili.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia (Sera, Bunge na Uratibu), Mhe. Ummy Nderiananga akitoa salamu katika uzinduzi wa baraza hilo uliofanyika Ukumbi wa Tume ya Taifa Uchaguzi (NEC) Machi 19, 2022 Jijini Dodoma.

“Baraza hili linazinduliwa kwa mara ya kwanza hivyo kukutana kwenu hapa iwe sehemu muhimu kwenu ya kuibua ubunifu katika mipango yenu na utekelezaji wa shughuli za ofisi kwa kutumia rasilimali zilizopo tuone namna gani tunaweza kubuni mambo mbalimbali katika mipango yetu kuhakikisha umma unapata huduma stahiki na kwa wakati,”amesema Mhe. Pindi.

Pia aliwapongeza kwa utendaji mwema wa kazi pamoja na ushirikiano hali inayosaidia shughuli za serikali kufanyika kwa wakati na viwango vinavyoridhisha katika utoaji wa huduma kwa wananchi.
Katibu Mkuu Ofsi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. John Jingu akieleza jambo kabla ya uzinduzi wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi hiyo katika Ukumbi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Machi 19, 2022 Jijini Dodoma.

Naibu Katibu Mkuu Ofsi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Bwa. Kaspar Mmuya akifafanua jambo kabla ya uzinduzi wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi hiyo katika Ukumbi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Machi 19, 2022 Jijini Dodoma.

“Nimefarijika kuona upendo na mshikamano uliopo kati ya Menejimeti na wafanyakazi wote wa ofisi hii Idara zote na upande wa sera kwa kweli nawapongeza sana na moyo huu wa kazi mlionao unajenga heshima ya Ofisi ya Waziri Mkuu ninawapongeza sana na Mheshimiwa Waziri Mkuu anatambua tuko hapa na amewapongeza sana,”alipongeza Mhe. Pindi.

Hata hivyo Mhe. Waziri Pindi aliwahimiza watumishi hao kuacha kufanya kazi kwa mazoea na kubadilika kifikra katika utendaji wa kazi akisisitiza upendo, bidii ya kazi , uwajibikaji na uadilifu kulingana na dira ya Ofisi hiyo ya kutoa huduma bora kwa umma na kufikia malengo ya serikali kwa kuratibu sekta zote kwa ufanisi na tija.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Balozi. Dkt. Pindi Chana akikata utepe kuzindua Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi hiyo katika Ukumbi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Machi 19, 2022 Jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Balozi. Dkt. Pindi Chana (wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi mbalimbali wa Ofisi hiyo na Wajumbe baada ya kuzindua Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi hiyo katika Ukumbi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Machi 19, 2022 jijini Dodoma. (Picha zote na OWM).

“Tuepuke kufanya kazi kwa mazoea kwa upande wa Menejimenti tunatakiwa kujipanga ipasavyo kusimamia upatikanaji wa haki za wafanyakazi na wafanyakazi kuzingatia wajibu wao kwa sababu suala la haki za wafanyakazi ni muhimu sana tukalipa kipaumbele,”Alieleza.

Wakati huohuo aliitaka Menejimenti kutataua kero za wafanyakazi kwa wakati hatua itakayosaidia kuleta mabadiliko katika maisha yao na ajira kwa ujumla na kuhakikisha wanakuwa na vitendea kazi vya kutosha vitakavyowawezesha kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi na kufanya kazi kwa kujituma.

“Vivile tuna wajibu wa kutatua kero za wafanyakazi kwa wakati kuleta mabadiliko ya maisha na ajira zao na ili yote haya yatimie ni muhimu uongozi utoe umuhimu mkubwa katika kipaumbele kuhakikisha upatikanaji wa vitendea kazi vya kutosha hususani katika bajeti hii ambayo ninaamini mtaijadili na kuweka vipaumbele vinavyotekelezeka,”alifafanua Mhe. Pindi.

Aidha uzinduzi wa Baraza hilo uliambatana na uchaguzi wa Katibu na Katibu Msaidizi ambapo Bi. Janet Shija alishinda nafasi ya Katibu wa Baraza la Wafanyakazi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu na Bwa. Edwald Bonafasi alishinda nafasi ya Katibu Msaidizi wa baraza hilo linaloongozwa na Mwenyekiti wake Dkt. John Jingu na Mwenyekiti Mwenza akiwa ni Bwa. Kaspar Mmuya.

Naye Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Ummy Nderiananga alipongeza juhudi kubwa zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan akitimiza mwaka mmoja tangu alipoingia madarakani Machi 19, 2021 kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano Hayati Dkt. John Pombe Magufuli aliyefariki Machi 17, 2021 akisema amekuwa mstari wa mbele kuhakikisha watanzania wanapata maendeleo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news