Waziri Bashungwa: Wakuu wa mikoa igeni mfano wa Mkoa wa Pwani kupitia Kituo cha Huduma za Pamoja (One Stop Center)

NA MWANDISHI MAALUM, OR-TAMISEMI

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais ofisi, TAMISEMI Mhe. Innocent Bashungwa amefurahishwa na Kituo cha Huduma za Pamoja ( One Stop Center) kilichoanzishwa kwenye Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani kwa ajili ya kutoa huduma za haraka kwa Wananchi wa Mkoa huo.
Akizungumza akiwa ziarani mkoani Pwani Mhe. Bashungwa amesema uwepo Huduma muhimu sehemu moja inamrahisishia mwananchi kutohangaika kuzunguka mji mzima kutafuta Ofisi mbalimbali za kutatua shida zake.

"Katika kituo hiki tunaona huduma mbalimbali zinapatikana katika eneo moja hapa tunawaona TRA, Uhamiaji, DAWASA, Magereza,TANROADS,TARURA, NEMC, TANESCO na wengine wengi sasa mwananchi wetu wanaweza kunaliza shida zao sehemu moja na sio ile mtu anafunga safari mpaka Ofisi fulani kisha unaambiwa suala hili sio la hapa nenda ofisi nyingine inachosha, lakini kwa hapa mahitaji mengi ya wananchi yanatatuliwa sehemu moja.

"Sasa niwatake wakuu wa mikoa yote nchini kuiga mfano huu na kuanzisha One Stop Center kwenye ofisi zao ili wananchi wa maeneo hayo waweze kupata huduma bora kwa urahisi na sio kusumbuka kama zamani,"amefafanua Mheshimiwa Waziri Bashungwa.

Kituo cha Huduma za Pamoja Mkoani Pwani kimeanza takribani mwezi mmoja sasa na kinajumuisha taasisi zote wezeshi kutoa huduma katika eneo moja.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news