Waziri Ndalichako asisitiza maadili ya Kiafrika muongozo wa SADC

NA LUSAJO MWAKABUKU,OWM-KVAU

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu, Mhe.Prof. Joyce L.Ndalichako amewataka wajumbe wa mkutano wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kuhakikisha katika mwongozo wa kulinda na kuzuia ajira mbaya kwa watoto ni vyema maneno yaliyotumika yakapatiwa tafsiri ili yaendane na maadili, utamaduni, na mazingira ya kiafrika.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako akichaangia jambo wakati wa Mkutano wa Mawaziri wa Kazi na Ajira kutoka Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC), Machi 30, 2022 Lilongwe nchini Malawi.
Matukio mbalimbali katika Mkutano huo wa Mawaziri wa Kazi na Ajira kutoka Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC), Machi 30, 2022 Lilongwe, nchini Malawi yakiendelea.

Waziri Ndalichako alitoa kauli hiyo Machi 30,2022 jijini Lilongwe Malawi alipokuwa akishiriki Mkutano wa Mawaziri wa Kazi na Ajira wa SADC waliokutana kujadili mambo mbalimbali juu ya sekta ya Kazi na Ajira ambapo katika kikao hicho ajenda 13 zinazohusu kuweka miongozo mbalimbali ya kusimamia masuala ya ukuzaji wa fursa za ajira, usimamizi wa viwango vya kazi, hifadhi ya jamii na usalama na afya mahala pa kazi.

Akitoa mchango wake, Profesa Ndalichako alisema suala la biashara ya ngono kwa mila na desturi ya nchi zetu za Afrika ni suala lisilokubalika, hivyo alisisitiza katika mwongozo huo isitafsiriwe kuwa biashara hiyo inakubalika kwa wasio watoto peke yake kwani kwa mazingira na tamaduni zetu za kiafrika biashara hiyo ni haramu.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali kutoka Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) mara baada ya Mkutano wa Mawaziri wa Sekta ya Kazi na Ajira uliofanyika Machi 30, 2022 Lilongwe nchini Malawi.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Wakurugenzi pamoja na Wataalamu alioambatana nao katika kikao hicho cha Mawaziri wa Kazi na Ajira kutoka Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC), Machi 30, 2022 Lilongwe nchini Malawi.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako (katikati) akisaini kitabu cha wageni alipotembelea Ubalozi wa Tanzania nchini Malawi. Kulia ni Balozi wa Tanzania nchini Malawi Mhe. Benedict Mashiba. Kushoto ni Mtendaji Mkuu wa Chama cha Waajiri Tanzania, Bi. Suzanne Ndomba.

Masuala mengine yaliyojadiliwa katika kikao hicho ni pamoja na kupitia rasimu ya Itifaki ya SADC ya Kazi na Ajira, Mwongozo wa kuanzisha Taasisi za Majadiliano ya Waajiri na Waajiriwa, Zana za Ufuatiliaji na Utoaji taarifa kuhusu utekelezaji wa Mpango wa Uhamaji Nguvukazi ndani ya SADC pamoja na kuanzisha mfumo wa taarifa za soko la ajira wa SADC.

Pia mijadala mingine ilifanyika juu ya Hali ya Utekelezaji na Uridhiaji wa Itifaki na Mikataba ya Shirika la Kazi Duniani na pia mkutano huu ulipokea taarifa kuhusu maandalizi ya ushiriki wa nchi za SADC katika Mkutano Mkuu wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) unaotaratijwa kufanyika Mwezi Juni, 2022.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news