Akiba Commercial Bank yafuturisha wateja Dar

NA DIRAMAKINI

BENKI ya Akiba Commercial imesema kuwa, inatambua na kuheshimu imani za wateja na wadau wake popote pale walipo nchini.
Mkurugenzi Mtendaji wa Akiba Commercial Bank Plc, Bw. Silvest Arumas akizungumza katika hafla ya futari iliyoandaliwa na benki hiyo jijini Dar es Salaam amesema, benki hiyo imeweka mipango mikakati kwa ajili ya wateja wake hasa katika kipindi hiki cha Ramadhan.
Mkurugenzi Mtendaji wa Akiba Commercial Bank Plc, Silvest Arumas akizungumza wakati wa hafla ya futari iliyoandaliwa na benki hiyo ikiwa ni sehemu ya jitihada za benki hiyo katika kuwajali wateja wake.

"Tunaupa umuhimu wa kipekee sana mwezi mtukufu wa Ramadhan sio tu kwa wateja na wadau bali ni kwa waislamu wote, kwani kama benki tunathamini na kujali kila dini, hivyo tumejikita kikamilifu katika mwezi huu wa Ramadhan kwa ajili ya kuwashika mkono ndugu zetu Waislam,"amesema.

Akiba Commercial Bank, imekuwa na utaratibu wao kama benki yenye kujali na kutambua umuhimu wa mwezi huu mtukufu wa Ramadhan kwa kuwaruhusu wafanyakazi kutoka kazini mapema kwa ajili ya ibada na matayarisho ya futari.
Baadhi ya wageni waalikwa wakifuturu katika hafla iliyoandaliwa na Akiba Commercial Bank ikiwa ni sehemu ya jitihada za benki hiyo katika kuwajali na kuwa karibu na wateja wao.

Pia Akiba Commercial Bank, imekuwa na utaratibu wakufanya hafla ya kuandaa futari kwa wateja wao kila mwaka kwa ajili ya kuwaunga mkono Waislamu katika funga yao pia kudumisha mahusiano kati ya wateja na benki yao pendwa.

Post a Comment

0 Comments