Ally Hapi:Mzee Kinana ni mtu safi, ana uwezo wa kipekee

NA MWANDISHI WETU

MKUU wa Mkoa wa Mara, Ally Hapi amesema kuwa, Abdulrahman Kinana ambaye jina lake limependelezwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ni mtu mwenye uwezo mkubwa na kuwataka kuachana na mambo ya nyuma.
Ameyasema hayo baada ya swali aliloulizwa na wanahabari nje ya Ukumbi wa Jakaya Kikwete unakofanyika Mkutano Mkuu wa CCM jijini dodoma ambapo amesema kuwa, mambo yaliyopita hayana msingi kwa sasa.

"Hakuna ubishi juu ya uwezo wa Mzee Kinana," ameeleza Hapi huku akifafanua kuwa Kinana ni mtu mwenye uwezo, maarifa na uzoefu mkubwa kwenye siasa na ni mwalimu kwa watu wengi kwenye chama hicho.

"Kama vijana ambao tunaendelea kujifunza kwenye siasa za chama mambo ya nyuma nadhani hayana msingi kwa sasa hivi,"amesema.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news