Balozi wa Tanzania nchini Austria awasilisha nakala za Hati za Utambulisho

Mheshimiwa Celestine Joseph Mushy ambaye ni Balozi wa Tanzania nchini Austria akiwasilisha nakala za Hati za Utambulisho kwa Mhe. Balozi Peter Launsky-Tieffenthal, Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje ya Austria leo Aprili 29,2022. Wakati akiwasilisha hati hizo, Katibu Mkuu alimpatia Balozi zawadi ya korosho ambazo zinalimwa na kubanguliwa Tanzania na Kampuni ya Austria inayojulikana kama Biotan Group Ltd yenye kiwanda kilichopo Mbagala jijini Dar es Salaam. Kampuni hiyo inazalisha na kubangua korosho ambazo ni 'organic'.

Post a Comment

0 Comments