Barrick yadhamini kongamano la wanafunzi vyuo vikuu

NA DIRAMAKINI

KAMPUNI ya Barrick imedhamini na kushiriki maonesho ya wanafunzi wa vyuo vikuu yaliyoandaliwa na Taasisi ya AISEC Tanzania, na kufanyika katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Kampasi ya Mlimani.
Baadhi ya watendaji waandamizi kutoka makampuni mbalimbali wakisikiliza hoja za wanafunzi wakati wa kongamano la Wanafunzi la AISEC lililofanyika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam chini ya udhamini mkuu wa Kampuni ya Barrick.
Mmoja wa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akiuliza swali wakati wa wa kongamano la Wanafunzi la AISEC lililofanyika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam chini ya udhamini mkuu wa kampuni ya Barrick.
Baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wakiwa katika picha ya pamoja na watendaji waandamizi wa makampuni mbalimbali wakati wa kongamano la Wanafunzi la AISEC lililofanyika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam chini ya udhamini mkuu wa kampuni ya Barrick. 

Kupitia maonyesho hayo wanafunzi huweza kujua jinsi taasisi mbalimbali nchini zinavyoendesha shughuli zake lengo kubwa ikiwa ni kuwajengea uwezo kwa kujifunza, kujitambua uwezo wao ni jinsi gani wanaweza kushiriki kutoa mchango wa kuendeleza taifa pindi wamalizapo masomo yao.
Baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wakiwa katika picha ya pamoja na watendaji waandamizi wa makampuni mbalimbali wakati wa kongamano la Wanafunzi la AISEC lililofanyika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam chini ya udhamini mkuu wa kampuni ya Barrick. 

Mameneja Waandamizi wa Barrick, walishiriki katika maonesho ya kongamano hilo ambapo walipata fursa kuzungumza na wanafunzi kuhusiana na kukabiliana na changamoto mbalimbali ikiwemo ajira,kuendeleza vipaji vyao pia wanafunzi walipata fursa kuelewa jinsi kampuni ya kimataifa ya Barrick, inavyoendesha shuguli zake sambamba na mpango wake wa ukuzaji wa vipaji kwa wafanyakazi wake.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news