SMZ, sekta binafsi kufanya jambo kuelekea Miaka 58 ya Muungano

NA KHADIJA KHAMIS-Maelezo

SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar ikishirikiana na Taasisi Binafsi imeandaa maonesho ya kibiashara yanayotarajiwa kufanyika Maisara jijini Zanzibar, ikiwa ni Shamramra ya kuelekea Maadhimisho ya miaka 58 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais (Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi), Mhe.Hamza Hassan Juma akitoa taarifa kwa waandishi wa Habari kuhusu maadhimisho ya miaka 58 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar huko Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Chukwani Zanzibar. (PICHA NA FAUZIA MUSSA –MAELEZO ZANZIBAR).

Maonesho haya yanatarajiwa kuanza Aprili hadi Mei 6 ambapo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Phillip Mpango anatarajiwa kuzinduwa maonyesho hayo.

Akitoa taarifa kwa waandishi wa Habari huko Baraza la Wawakilishi Chukwani , Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais (Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi ) Mhe. Hamza Hassan Juma amesema harakati za ujenzi wa miunombinu ya maonesho hayo inaendelea katika viwanja vya Maisara .

Amesema jumla ya Shilingi milioni 250 zinatarajiwa kutumika katika maadhimisho hayo ambazo zitatolewa na wafanya biashara ambao watashiriki katika maonyesho hayo.

Aidha, alisema Sherehe za Maadhimisho hayo zitaanza kwa Kongamano ambalo linatarajiwa kufanyika tarehe 20 mwezi huu katika Ukumbi wa Gorden Tulip, Uwanja wa Ndege Zanzibar na Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa ni Makamu wa Pili wa Rais Mheshimiwa Hemed Suleiman Abdulla.

Alifafanua kuwa kongamano hilo litazungumzia suala zima la Muungano ikiwemo mafanikio na changamoto pamoja na kuelezea historia za Waasisi wa Muungano huo.

Mhe. Hamza ametoa wito kwa Wananchi kujitokeza kwa wingi katika maonyesho hayo licha ya kupata fursa za Biashara pia watapata ufafanuzi wa taarifa mbalimbali za muungano.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news