Bunge laahirishwa hadi Mei 5,2022 kupisha Sikukuu ya Idd el Fitr

NA DIRAMAKINI

SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Tulia Akson ameahirisha mkutano wa Bunge hadi Mei 5, 2022 saa tatu asubuhi.

Imeelezwa sababu ya kuahirishwa kwa siku zote ni kutokana na kutokuwa na uhakika wa mwanadamo wa mwezi ambao utafanya uwepo wa Sikukuu ya Idd el Fitr kwa waumini wa dini ya Kiislamu inayoendana na mwandamo wa mwezi.
Mheshimiwa Spika amesema kulingana na tangazo la Mufti wa Tanzania kuwa huenda sikukuu ikawa kati ya Jumatatu au Jumanne, anaona busara kuahirisha Bunge hadi Alhamisi kwa kuwa hakutakuwa na siku ya kukutana tena.

“Waheshimiwa wabunge, kutokana na tangazo la Mufti ni ngumu kusema tunaweza kukutana tena na kupeana matangazo, kwa hiyo naona vema tuheshimu hilo na kwa hiyo naahirisha shughuli za Bunge hadi Alihamisi saa tatu asubuhi,” amesema Mheshimiwa Spika.

Post a Comment

0 Comments