Maagizo ya Waziri Bashungwa kwa MA-DC kuhusu zao la kahawa

NA OR-TAMISEMI

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Mhe. Innocent Bashungwa amewaagiza wakuu wa wilaya mkoani Kagera kusimamia kikamilifu maelekezo ya Serikali iliyoyatoa kwenye zao la kahawa na kuhakikisha bei wanayolipwa wakulima inakuwa sawa na bei ya soko katika msimu husika.

Mheshimiwa Bashungwa ametoa maelekezo hayo katika mkutano wa wadau wa maendeleo wilayani Karagwe mkoani Kagera wa kujadili ufungamanishaji wa kilimo na uchakataji malighafi viwandani uliofanyika Aprili 28, 2022.
“Msimu huu Mkoa wa Kagera utakuwa kanda maalum ili kuhakikisha bei ya kahawa ambayo mkulima analipwa inakuwa sawa na bei ya soko katika mwaka husika,” amesema Bashungwa.

Bashungwa amesema, Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa katika ziara yake wilayani Karagwe alitoa maelekezo kuondolewa kwa tozo 42 kati ya 47 ambazo walikuwa wanatozwa wakulima wa kahawa wa Mkoa wa Kagera.
Aidha, Bashungwa amesema Serikali ya Awamu ya Sita inayongozwa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan inataka mkulima anufaike na jasho lake katika kilimo hususani kahawa.
Kwa upande wake, Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe wakati akiongea na wadau hao kwa njia ya simu amesema Serikali imebadilisha Mfumo wa Chama Kikuu kujikusanyia mazao na kuwafanya wanunuaji wengine kupita kwao, hivyo kwa sasa ushindani wa bei utaanzia kwenye vyama vya msingi.

Pia amemwagiza Mkurugenzi wa Bodi ya Kahawa na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Mazao wa Wizara ya Kilimo na timu yake kukaa Mkoa wa Kagera katika msimu wote kusimamia maelekezo ya Serikali iliyoyatoa kwenye zao la kahawa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news