Madiwani Moshi wamng'oa Meya madarakani

NA DIRAMAKINI

MADIWANI wa Manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro wamepiga kura ya kumuondoa meya wa wa manispaa hiyo, Juma Raibu madarakani kutokana na tuhuma mbalimbali zinazomkabili.
Kura 18 zimemuondoa madarakani Aprili 11,2022 Meya huyo kutokana na tuhuma nne zinazomkabili ikiwemo tuhuma za rushwa katika vibali vya ujenzi majengo katika halmashauri ya manispaa hiyo.

Tuhuma nyingine zinazomkabili ni matumizi mabaya ya madaraka pamoja na mwenendo mbaya wa ukosefu wa adabu dhidi ya madiwani wenzake.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Moshi, Rashid Gembe amesema, kura 28 zilizopigwa na madiwani hao kura 18 zilikuwa za ndiyo na kura 10 zikisema hapana jambo ambalo lilihitimishwa kwa mujibu wa kanuni na Meya huyo kung’olewa madarakani.

Post a Comment

0 Comments