Mapato hoi kwa OR-TAMISEMI,yalazwa 2-0 hadi fainali

NA FRED KIBANO

TIMU ya mpira wa miguu ya Ofisi ya Rais TAMISEMI imefanikiwa kutinga fainali ya michuano ya kombe la Mei Mosi 2022 baada ya kuitandika Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) bao 2- 0 jijini Dodoma leo.

Wachezaji Lewis Masekage na Godfrey Miller ndio waliopachika magoli katika kipindi cha pili cha mchezo huo na kuifanya OR-TAMISEMI kuibuka na ushindi mnono dhidi ya wapinzani wao timu ya TRA katika Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.

Michezo miwili ya nusu fainali ilikuwa kati Maliasili na Ulinzi ambapo timu ya Maliasili ilifanikiwa kupata goli 1-0 dhidi ya ulinzi katika uwanja huo huo jijini Dodoma. 

Katika hatua ya fainali ambayo itafanyika Mei 2, 2022 jijini Dodoma katika Uwanja wa Jamhuri ambapo miamba ya soka OR-TAMISEMI na wenzao MALIASILI watacheza kuhitimisha mashindano ya Kombe la Mei Mosi 2022.
Aidha, hapo kesho timu mbili za Ulinzi na TRA zitamenyana uwanjani katika dimba la Uwanja wa Jamhuri-Chama cha Mapinduzi jijini Dodoma ili kumpata mshindi wa tatu. 

Jumla ya timu zipatazo 32 zimeshiriki mashindano hayo katika hatua za mtoano wa makundi tangu kuanza mashindano hayo takribani wiki moja iliyopita.

Post a Comment

0 Comments