Mbaroni kwa mauaji ya mlinzi jijini Arusha

NA DIRAMAKINI

PENDAEL Mollel ambaye ni mfanyabiashara maarufu wa madini ya Tanzanite jijini Arusha na wenzake watatu, wamekamatwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kumteka mlinzi kisha kumpiga na kumuua Aprili 19,2022.
Mollel akiwa na wanzake wanadaiwa walifika eneo la Burka karibu na Uwanja wa Ndege wa Arusha kumchukua, Stephen Jimmy (43) kwenye nyumba aliyokuwa akilinda, inayomilikiwa na Mtanzania mwenye asili ya Somalia, Mahmudu Mohamed siku ya Aprili 19, 2022 majira ya saa moja usiku na kutenda mauji hayo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Justin Masejo amethibitisha kukamatwa kwa mfanyabiashara huyoAprili 22, 2022 na kueleza kuwa, mtuhumiwa alikamatwa Moshi mkoani Kilimanjaro alikokimbilia kujificha baada ya mauaji hayo.

Amesema kuwa, watuhumiwa wote wapo rumande Kituo Kikuu cha Polisi Arusha, kwa mahojiano na kuna watuhumiwa wengine wanatafutwa, ili kuunganishwa kwenye tukio hilo.

Pia amesema, kwa sasa hawezi kuzungumza kwa undani, zaidi ya kujua kuwa watuhumiwa wako rumande, ila baada ya siku moja ama mbili wahusika wakikamilisha kutoa maelezo na wengine kukamatwa atatoa taarifa kwa vyombo vya habari juu ya tukio zima.

"Ninachoweza kusema kwa sasa ni kukiri kuwa mfanyabiashara wa madini ya Tanzanite, Pendael Mollel, tumemkamata Moshi kwa tuhuma za mauaji, wenzake watatu wamekamatwa Arusha,”amesema Kamanda Masejo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news