Paul Makonda ataja makundi matano anayodai yanataka kumuua

NA DIRAMAKINI

ALIYEWAHI kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mheshimiwa Paul Makonda amesema kuwa, kuna mkakati unaoratibiwa na makundi matano kwa ajili ya kuangamiza maisha yake.
Mheshimiwa Makonda ameyaeleza hayo kupitia ukurasa wake wa Instargram huku akiyataja makundi hayo na kujiuliza mambo mawili.

"Nafahamu kuna mkakati unaoratibiwa na makundi matano kuangamiza maisha yangu;
1) WAUZA MADAWA YA KULEVYA
2)WANUFAIKA NA MADAWA YA KULEVYA
3) MASHOGA
4)WANAOKESHA USIKU KUCHA KUTAFUTA KULIPA KISASI KWA WASAIDIZI WA DR MAGUFULI.
5) WALIOWAHI KUWA SEHEMU YA ……. Nafahamu pia juu ya mbinu zinazoandaliwa ili kuniuwa kwa faida ya familia zao pamoja na kutengeneza mashaidi wa uongo ili mnipe kesi ya uhujumu uchumi.

Mambo mawili najiuliza
1)PAMOJA NA KAZI ZOTE NZURI NILIZOZIFANYA KWA CHAMA CHANGU,SERIKALI YANGU NA WANANCHI WA DAR HAYA NDIYO MALIPO YAKE?
2)Hakika ukiwa mtumishi mwaminifu unaetetea haki za wanyonge tena ukitokea kwenye familia masikini haya ndiyo malipo yake ?

"MTU aliyejemga hospitali, aliyejenga ofisi za CCM, magari ya polisi, ofisi za walimu, vituo vya polisi, shule za sekondari mpaka na msingi, kutibu wagonjwa mpaka meli kuja Tanzania,kuhudumia makundi mbalimbali mpaka kuiunganisha Serikali na viongozi wa dini. Leo hii naonekana eti natakiwa kunyongwa.

"Pamoja na kwamba lipo kundi kwenye mitandao linalolipwa ili kuwaanda watanzania pale watakaponikamata ionekane ni sawa. Hakika ipo siku walemavu, yatima, wajane na waliotamani watoto WAO wasife kwa MADAWA ya KULEVYA SAUTI ZAO ZITASIKIKA.#Ukiona maji yametulia jua kina ni kirefu,"ameeleza Makonda.
Paul Makonda ni nani?

Paul Makonda ambaye amewahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, alizaliwa Februari 15,1982 katika Zahanati ya Kolomije wilayani Misungwi, Mwanza.

Amewahi kukaririwa akisema kuwa, yeye ni mtoto wa kipekee wa kiume katika familia ya Mzee Makonda na Suzan.

Paul Makonda alitoka katika familia ya kawaida ambayo mama yake alisoma hadi darasa la saba na baba yake hakufanikiwa kusoma.

Paul Makonda huwa anaamini kuwa, hatua aliyofikia ni neema ya Mungu kwake ikizingatiwa aliweza kupata heshima kubwa katika historia ya maisha yake, licha ya kutoka katika familia duni.

Aidha,familia yake pia ilibarikiwa kupata mtoto wa kike,lakini kwa bahati mbaya alifariki akiwa na umri wa mwaka mmoja na miezi sita tangu azaliwe.

Paul Makonda alipata elimu ya msingi katika Shule ya Msingi Kolomije na baadaye akajiunga na masomo ya sekondari hadi kidato cha nne.

Kutokana na changamoto ya kipato iliyoikabili familia yao wakati huo, hakuweza kwenda sekondari, lakini alijiunga na chuo cha uvuvi cha Mbegani kilichopo Bagamoyo kwa ngazi ya cheti na stashahada. Baadaye alijiunga na Muccobs mjini Moshi kwa shahada yake ya kwanza.

Akiwa ni mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), baada ya kumaliza elimu yake ya ngazi ya Shahada alihamia Dar es salaam akitokea Moshi.

Mwaka 2015 aliteuliwa na Rais wa Awamu ya Nne, Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete kuwa,Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni kwa maana ya Februari 18.

Aidha, Machi 13, 2016 Rais mpya wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Serikali ya Awamu ya Tano, hayati Dkt.John Pombe Magufuli alimteua tena kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.

Post a Comment

0 Comments