Peter Nwachukwu, mume wa marehemu mwimbaji wa nyimbo za injili wa Nigeria Osinachi Nwachukwu akamatwa

LAGOS-Mume wa marehemu mwimbaji wa nyimbo za Injili wa Nigeria Osinachi Nwachukwu amekamatwa kufuatia kifo chake, vyombo vya habari vya nchini humo vimeripoti.
Osinanchi mwenye umri wa miaka 42 alifariki Ijumaa iliyopita akiwa hospitalini katika mji mkuu, Abuja.

Msemaji wa polisi mjini humo amenukuliwa na tovuti za Daily Trust and Punch akithibitisha kukamatwa kwa Peter Nwachukwu baada ya malalamiko kutoka kwa kakab yake mwimbaji huyo.

Haijabainika iwapo Bw. Nwachukwu ametoa maoni yake kuhusu kukamatwa kwake.

Osinachi alipata umaarufu 2017 kwa wimbo wa injili Ekwueme aliouimba na Prospa Ochimana.

Pia alikuwa mwimbaji mkuu Dunamis International Gospel Centre.

Post a Comment

0 Comments