Rais Samia asisitiza ushirikiano na vyama vyote vya siasa

NA DIRAMAKINI

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ametoa wito kwa vyama vya siasa na wadau wengine wa siasa kufanya majadiliano na kutoa mapendekezo ambayo yataleta maridhiano, haki na amani hapa nchini.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD), Zitto Kabwe na Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM-Bara), Abdulrahman Kinana wakitoka nje ya ukumbi wa mikutano wa Hazina jijini Dodoma.

Mheshimiwa Rais Samia ametoa rai hiyo leo Aprili 5,2022 wakati akifungua mkutano wa Kitaifa wa haki, amani na maridhiano unaofanyika katika Ukumbi wa Hazina jijini Dodoma.

Pia amevitaka vyama hivyo kufanya majadiliano kwa kuzingatia hali ya siasa, uchumi na mazingira halisi ya nchi kwa manufaa ya Watanzania wote bila kujali itikadi za vyama vyao.

Amesema kuwa, Tanzania ilichagua mfumo wa vyama vingi ili kuiwezesha kupata maendeleo kwa haraka, hivyo amewahakikishia kuwa, Serikali itashirikiana na vyama vya siasa hususani katika masuala ya kisera na kisheria ili kujenga nchi.

Wakati huo huo, Mheshimiwa Rais Samia amekiagiza Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) kuangalia mfumo wa wajumbe wanaounda taasisi hiyo ili kujumuisha wawakilishi kutoka ngazi zote za kisiasa na kuhakikisha wanafikia malengo yanayokusudiwa.

TCD ni taasisi isiyo ya kiserikali iliyoundwa na vyama vya siasa vyenye uwakilishi kwenye Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Baraza la Wawakilishi Zanzibar na Baraza la Madiwani iliyosajiliwa mwaka 2005.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news