Rais Samia atangaza siku mbili za maombolezo ya Kitaifa kufuatia kifo cha Mwai Kibaki

NA DIRAMAKINI

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, ametangaza siku mbili za maombolezo ya kitaifa kufuatia kifo cha Rais mstaafu wa Kenya, Mhe. Emilio Mwai Kibaki, kilichotokea Aprili 21, 2022 jijini Nairobi.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais (Ikulu), Zuhura Yunus imeeleza kuwa, maombolezo hayo yataanza leo Aprili 29 hadi Aprili 30, 2022.

"Katika kipindi chote cha maombolezo, bendera zote zitapepea nusu mlingoti nchini Tanzania zikiwemo kwenye balozi zetu pia. 

"Rais Samia amewaomba Watanzania wote kuungana na wenzetu wa nchi jirani ya Kenya katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na aliyekuwa kiongozi wao nchini humo,"imeeleza sehemu ya taarifa hiyo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news