Rais Samia:Mfuko wa Maendeleo ya Kilimo uanzishwe

NA DIRAMAKINI

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ameiagiza Wizara ya Kilimo kushirikiana na Wizara ya Fedha na Mipango, kuanzisha Mfuko wa Maendeleo ya Kilimo nchini.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe wakati akumuelezea kuhusu bidhaa mbalimbali za kilimo kabla ya kuzindua na kugawa vitendea kazi kwa Maafisa Ugani wa Kilimo nchini katika ukumbi wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma leo Aprili 4, 2022. (Picha na Ikulu).

Rais Samia ametoa agizo hilo leo Aprili 4, 2022 wakati akizindua ugawaji wa vitendea kazi vya maafisa ugani kilimo ikiwemo pikipiki, vifaa vya kupima afya ya udongo, simu janja na visanduku vya ufundi kwenye hafla iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu akiwa na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe, Naibu Waziri wa Kilimo Antony Mavunde pamoja na Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Daniel Chongolo wakati akikata utepe kuashiria uzinduzi wa ugawaji wa pikipiki 7000 kwa ajili ya Maafisa Ugani Kilimo wa nchi nzima katika hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma leo.

Rais Samia amesema, mfuko huo utachangiwa na tozo maalum kwenye mazao ya kilimo, Mfuko Mkuu wa Sefikali na wadau wa maendeleo.

Amesema, mfuko huo utakuwaa na majukumu ya kugharamia pembejeo za kilimo kama ilivyofanyika kwenye korosho, pamba na tumbaku ili mfuko huo utumike kama ruzuku pindi pembejeo zinapopanda bei.
Pia ameiagiza wizara hiyo na Ofisi ya Rais-Utumishi kupitia upya na kuufanyia mabadiliko muundo wa Tume ya Umwagiliaji ili kuhakikisha inakuwa na ofisi katika kila wilaya.

Kwa upande mwingine, Rais Samia ameagiza mashamba yote ambayo yapo chini ya Ofisi ya Msajili wa Hazina kufufuliwa na kuaza kutumika kwa kushirikiana na sekta binafsi kupitia mfumo wa kukodisha ardhi kwa muda mrefu.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe wakati akielezea kuhusu vitendea kazi kwa Maafisa Ugani Kilimo kabla ya uzinduzi katika ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma leo.

Aidha, Rais Samia ameitaka Wizara ya Kilimo kuweka msukumo kwenye uzalishaji wa mazao ya chakula na kuwa ya kibiashara, ikiwemo mazao ya mboga mboga pamoja na mazao ya kimkakati ili kukidhi mahitaji ya ndani na kuuza ziada nje ya nchi.

Rais Samia amesema, Sekta va Kilimo nchini imeendelea kukuza uchumi na kuleta maendeleo kwa taifa ambapo kwa mwaka 2020 sekta ya kilimo ilikua kwa asilimia 4.9 kuchangia kwa asilimia 26.9 katika pato la taifa, kuchangia kwa asilimia 61.1 katika kutoa Ajira kwa Watanzania na kuchangia kwa asilimia 65 ya malighafi za viwandani. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiangalia mchele uliowekwa kwenye kifungashio kwa ajili ya kupelekwa sokoni katika Maonesho yaliyofanyika nje ya ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma leo.Kushoto ni Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania heshimiwa Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe wakati akielezea kuhusu vitendea kazi kwa Maafisa Ugani Kilimo kabla ya uzinduzi katika ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma leo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu akimkabidhi mfano wa Ufunguo wa Pikipiki Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe mara baada ya kuzindua ugawaji wa pikipiki hizo 7,000 kwa ajili ya Maafisa Ugani nchini.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu akiwasha pikipiki mara baada ya kuzindua ugawaji wa pikipiki hizo 7000 kwa ajili ya Maafisa Ugani nchini.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka mara baada ya kuzindua ugawaji wa pikipiki hizo 7000 kwa ajili ya Maafisa Ugani nchini katika hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma leo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news