Utabiri wa hali ya hewa Tanzania saa 24 zijazo/Weather forecast April 4th,2022 starting 21:00 tonight

*MAWINGU KIASI, MVUA NA NGURUMO ZINATARAJIWA KATIKA MAENEO MACHACHE

NA GODFREY NNKO

UTABIRI wa hali ya hewa wa saa 24 zijazo kuanzia saa 3 usiku wa leo Aprili 4,2022 umeletwa na mchambuzi Godfrey Kazinja kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA).
Kwa mujibu wa TMA, mikoa ya Ruvuma, Kigoma, Katavi, Rukwa, Songwe, Mbeya, Njombe, Mwanza, Kagera, Geita na Shinyanga inatarajiwa kuwa na hali ya mawingu kiasi, mvua na ngurumo katika maeneo machache na vipindi vya jua.

Mikoa ya Lindi, Mtwara, Kusini mwa Mkoa wa Morogoro inatarajiwa kuwa na hali ya mawingu kiasi, mvua nyepesi katika maeneo machache na vipindi vya jua.

Visiwa vya Unguja na Pemba, Mikoa ya Dodoma, Singida, Dar es Salaam, Tanga, Tabora, Simiyu, Mara, Iringa, Kaskazini mwa Mkoa wa Morogoro, Manyara, Kilimanjaro, Arusha na Pwani (ikijumuisha Visiwa vya Mafia) inatarajiwa kuwa na hali ya mawingu kiasi na vipindi vya jua.

Aaidha, kwa mujibu wa TMA upepo wa Pwani unatarajiwa kuvuma kwa kasi ya kilomita 20 kwa saa kwa Pwani yote kutoka Mashariki kwa Pwani ya Kaskazini na kutoka Kaskazini Mashariki kwa Pwani ya Kusini.

Hali ya Bahari: Inatarajiwa kuwa na mawimbi madogo ambapo matarajio kwa siku ya Jumatano ya Aprili 6,2022.

TANZANIA WEATHER FORECAST 04.04.2022:ISOLATED THUNDERSHOWERS ARE EXPECTED OVER FEW AREAS
Weather forecast for the next 24 hours starting tonight at 9:00 p.m on 04.04.2022 as presented by weather analyst Joyce Makwata from Tanzania Meteorological Authority (TMA).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news