Simba SC yaivutia kasi Yanga SC kileleni

NA DIRAMAKINI

WEKUNDU wa Msimbazi, Simba SC wameendelea kuivutia kasi Yanga SC kileleni mwa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara baada ya kufikisha alama 40 dhidi ya 51 walizonazo Wanajangwani.
Ni baada ya kucheza mchezo wa 18, ingawa inabaki nafasi ya pili ilizidiwa alama 11 na watani, Yanga ambao pia wamecheza mechi moja zaidi.

Alama hizo zimeongezeka leo Aprili 7, 2022 baada ya kujibebea alama tatu ugenini dhidi ya Coastal Union katika dimba la Mkwakwani jijini Tanga.

Mabao ya Simba SC yamefungwa na winga Mghana, Bernard Morrison dakika ya 40 na mshambuliaji Mnyarwanda, mzaliwa wa Uganda, Meddie Kagere dakika ya 90 huku Coastal Union likiwa limefungwa na mshambuliaji Mnigeria, Victor Patrick Akpan dakika ya 78.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news