TANZIA:Mwanafunzi Chuo Kikuu Iringa afariki

NA DIRAMAKINI

UONGOZI wa Chuo Kikuu cha Iringa,umesema umepokea kwa masikitiko taarifa ya kifo cha mwanafunzi wake, Hashim Komgisa Mzalilehi kupitia Idara ya Elimu Kitivo cha Sayansi na Elimu.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Afisa Habari na Masoko katika Chuo Kikuu cha Iringa (UoI).

"Uongozi unautaarifu Umma wa chuo kuwa msiba umetokea Jumamosi tarehe 23,4,2022 huko Mwanza, na mazishi (maziko) yatafanyika leo Jumapili 24,4,2022 Mwanza Sengerema.

"Uongozi wa chuo, unawapa pole wafiwa wote, na Mungu aipumzishe roho ya marehemu mahala pema peponi,"imeeleza taarifa hiyo.

Post a Comment

0 Comments