TFF:Mwisho wa kurudisha fomu za leseni kwa klabu ni Aprili 25

NA DIRAMAKINI

SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limezikumbusha klabu kwamba tarehe ya mwisho ya kurudisha fomu za maombi ya leseni za klabu ni Aprili 25, 2022.
"Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), linazikumbusha Klabu za Ligi Kuu ya NBC, Championship na First League kujaza fomu za maombi ya leseni za klabu msimu wa 2022/2023 zinaendelea kutolewa.

"Fomu zinapatikana makao makuu ya TFF, Karume Ilala kwenye ofisi ya Meneja wa Leseni za Klabu bila malipo yoyote, pia unaweza kupakua kwwenye tovuti yetu ya www.tff.or.tz,"imefafanua taarifa ya TFF.

Post a Comment

0 Comments