Utabiri wa hali ya hewa Tanzania saa 24 zijazo/Weather forecast April 12th,2022 starting 21:00 tonight

*ANGALIZO LA VIPINDI VYA MVUA KUBWA: VIPINDI VYA MVUA KUBWA VINATARAJIWA KATIKA BAADHI YA MAENEO YA UKANDA WA PWANI YOTE YA BAHARI YA HINDI (MIKOA YA MTWARA, LINDI, DAR-ES-SALAAM, TANGA NA PWANI (IKIJUMUISHA VISIWA VYA MAFIA), PAMOJA NA VISIWA VYA UNGUJA NA PEMBA

NA GODFREY NNKO

UTABIRI wa hali ya hewa wa saa 24 zijazo kuanzia 3:00 usiku leo Aprili 12, 2022 unawasilishwa na mchambuzi Godfrey Kazinja kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA).Kwa mujibu wa TMA, Ukanda wa Pwani ya bahari ya Hindi mikoa ya Lindi, Mtwara, Dar es Salaam, Tanga, Pwani (ikijumuisha Visiwa vya Mafia) pamoja na Visiwa vya Unguja na Pemba inatarajiwa kuwa na mvua na ngurumo.

Mikoa ya Morogoro, Kigoma, Ruvuma, Kagera, Geita, Shinyanga, Mwanza, Simiyu na Mara inatarajiwa kuwa na mawingu kiasi, mvua na ngurumo.

Aidha, kwa mujibu wa TMA mikoa ya Kilimanjaro, Arusha, Rukwa, Songwe, Iringa, Mbeya na Njombe inatarajiwa kuwa na hali ya mvua nyepesi kwa maeneo machache.

Wakati huo huo, kwa mujibu wa TMA mikoa ya Katavi, Tabora, Manyara, Dodoma na Singida inatarajiwa kuwa na vipindi vya jua.

TANZANIA WEATHER FORECAST 12.04.2022:HEAVY PRECIPITATION AT TIMES ARE EXPECTED OVER SOME AREAS OF THE ENTIRE COAST OF THE INDIAN OCEAN (MTWARA, LINDI, TANGA, DAR-ES-SALAAM AND PWANI REGIONS (NCLUDING MAFIA ISLES), TOGETHER WITH UNGUJA AND PEMBA ISLES)Weather forecast for the next 24 hours starting 21:00 tonight 12.04.2022, presented by weather analyst Godfrey Kazinja from Tanzania Meteorological Authority (TMA).

Post a Comment

0 Comments