Utabiri wa hali ya hewa Tanzania saa 24 zijazo/Weather forecast April 17th,2022 starting 21:00 tonight

*MVUA NA NGURUMO INATARAJIWA KATIKA MAENEO MENGI YA NCHI

NA GODFREY NNKO

UTABIRI wa hali ya hewa kwa saa 24 zijazo kuanzia saa tatu usiku leo Aprili 17, 2022 unaletwa na Tabu Kwedilima kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA).
Kwa mujibu wa TMA, Tabora, Kigoma, Katavi, Morogoro, Dar es Salaam, Pwani(visiwa vya Mafia), Tanga, Kagera, Geita, Simiyu, Mwanza, Shinyanga, Mara na Visiwa vya Unguja na Pemba inatarajiwa kuwa na mvua na ngurumo kwa maeneo machache na vipindi vya jua.

Aidha, Manyara, Kilimanjaro na Arusha inatarajiwa kuwa na mvua kwa maeneo machache na jua huku Ruvuma, Lindi, Mtwara, Rukwa, Songwe, Mbeya, Iringa na Njombe ikitarajiwa kuwa na mvua nyepesi na jua.

Wakati huo huo Dodoma na Singida inatarajiwa kuwa na jua. Aidha, upepo wa bahari unatarajiwa kuvuma kwa kasi ya kilomita 30 kwa saa kwa Pwani yote kutoka Kusini kwa Pwani ya Kaskazini na kutoka Kusini Mashariki kwa Pwani ya Kusini huku hali ya bahari ikitarajiwa kuwa na mawimbi makubwa kiasi.

TANZANIA WEATHER FORECAST 17.04.2022:THUNDERSHOWERS IS EXPECTED OVER MOST AREAS OF THE COUNTRY
Weather forecast for the next 24 hours presented by analyst Mohamedi Hamisi from Tanzania Meteorological Authority (TMA).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news