Utabiri wa hali ya hewa Tanzania saa 24 zijazo/Weather forecast April 6th,2022 starting 21:00 tonight

*MAWINGU KIASI, MVUA NA NGURUMO ZINATARAJIWA KATIKA MAENEO MACHACHE

NA GODFREY NNKO

UTABIRI wa hali ya hewa wa saa 24 zijazo kuanzia saa tatu usiku leo Aprili 6,2022 unaletwa na mchambuzi, Magreth Massawe kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA).
Mikoa ya Ruvuma,Kagera, Geita, Kigoma, Katavi, Rukwa, Songwe, Mbeya, Mwanza, Shinyanga na Njombe inatarajiwa kuwa na mvua na ngurum kwa maeneo machache na vipindi vya jua.

Aidha, kwa mujibu wa TMA. Mara na Simiyu inatarajiwa kuwa na ngurumo kwa maeneo machache na jua huku Lindi, Mtwara na Kusini mwa Mkoa wa Morogoro ikitarajiwa kuwa na mvua nyepesi kwa maeneo machache na vipindi vya jua.

Tabora, Iringa, Visiwa vya Unguja na Pemba, Dodoma, Singida, Dar es Salaam, Tanga, Kaskazini mwa Mkoa wa Morogoro, Manyara, Kilimanjaro, Arusha na Pwani (ikijumuisha Visiwa vya Mafia) inatarajiwa kuwa na vipindi vya jua.

Pia kwa mujibu wa TMA,upepo wa Pwani unatarajiwa kuvuma kwa kasi ya kilomita 20 kwa saa kwa Pwani yote; kutoka Mashariki kwa Pwani ya Kaskazini na kutoka Kaskazini Mashariki kwa Pwani ya Kusini. Huku hali ya bahari ikitarajiwa kuwa na mawimbi madogo.

WEATHER FORECAST FOR THE NEXT 24 HOURS STARTING AT 9.00 P.M:ISOLATED THUNDERSHOWERS ARE EXPECTED OVER FEW AREAS


Post a Comment

0 Comments