Wamachinga Dar waweka taarifa sawa

NA DIRAMAKINI

CHAMA cha Wamachinga Mkoa wa Dar es Salaam, wamekanusha taarifa iliyosambaa mtandaoni iliyotolewa na Shirikisho la Umoja wa Machinga Tanzania kuhusu kutoshiriki kwa wamachinga kwenye Maonesho ya Biashara yanayotarajia kufanyika hivi karibuni kwenye viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Machinga Mkoa wa Dar es Salaam, Bw.Namoto Yusuph amesema wamesikitishwa na taarifa hiyo ambayo ilisema mwaka huu hakutakuwa na ushiriki wa machinga kwenye maonyesho ya Biashara ya Kimataifa Dar es salaam na kama kuna mtu atahitaji kushiriki basi atahitajika kulipia shilingi milioni moja kama taasisi nyingine.

Amesema kuwa, taarifa hiyo imeleta taharuki kwa wananchi walio wengi hivyo taarifa kama hiyo ingetakiwa itolewe na Mamlaka ya Biashara TAN TRADE.

"Niseme kuwa sisi kama wamachinga wa Mkoa wa Dar es Salaam tulishiriki mwaka jana katika maonyesho tulikipia kiingilio cha laki moja na tukapewa meza kiti na kitambulisho hivyo taarifa hizo zilizosambaa siyo za ukweli zipuuzwe kiingilio hakijapanda kufikia kiasi hicho,"amesema Namoto.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Chama cha Wamachanga Mkoa wa Dar es Salaam, Bw.Masoudy Chauka ametoa taarifa kwa viongozi wote wa wamachinga kuwepo kwa mfumo data wa machinga pamoja na mfumo wa Saccos ili kuwatambua wamachinga wote na kutatua changamoto zinazowakabili.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news