Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) yatoa rai kwa waandishi wa vitabu ya kiada

NA DIRAMAKINI

MKURUGENZI Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET), Dkt.Aneth Komba amewahimiza wataalamu wa uandishi wa vitabu vya kiada kutumia uwezo wao wote ili waweze kuandika vitabu bora kwa ajili ya maslahi ya taifa.  Ameyasema hayo leo Aprili 21,2022 kwenye ufunguzj wa kazi ya Uhariri wa Maudhui wa aina 43 za visawidi vya vitabu vya kiada kidato cha kwanza hadi cha sitana uhariri wa lugha viongozi vitano vya walimu vya darasa la tano uliofanyika katika ukumbi wa shule ya Sekondari Morogoro Mjini.

“Wataalamu ninawaomba sana mtumie uwezo na uzoefu wenu wote katika kuifanya kazi hii ya uhariri ili kuwezesha kupatikana vitabu ambavyo vitakuwa bora,”amesema Dkt.Komba.
Ameeleza pia uhariri huo unahitaji kufanyika kwa uaminifu mkubwa kwa muda wote na haipaswi kabisa mtaalamu yoyote kusambaza nakala yoyote nje ya kikao kazi husika.

Pamoja na mambo mengine, amewataka wataalamu kuwa huru katika uhariri wao, na kama kuna sehemu itahitajika kubadilishwa kwa kuongeza ama kupunguza jambo hata kama halipo kwenye mhtasari ilimradi viendane na maendeleo ya teknolojia, ifanyike ivyo ili kukidhi lengo la ujifunzaji.

Pia amesema wakati wa uhariri wataalamu wakubaliane juu ya maboresho yoyote badala ya Kila mtaalamu kuboresha kitu kulingana na upenzi wake binafsi.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Idara ya Ubunifu na Uboreshaji wa Vifaa vya Kielimu, Bw.Fixon Mtelesi amewasihi watalaamu kutumia lugha rahisi na ya kueleweka kwa wanafunzi kulingana na kiwango chao cha elimu, lakini pia maudhui na mifano iliyomo kwenye vitabu hivyo isadifu mazingira halisi ya wanafunzi.

Taasisi ya Elimu Tanzania inatarajia kukamilisha zoezi la uandishi wa vitabu vya kiada ndani ya mwezi wa sita mwaka huu wa 2022.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news