NA TITO MSELLEM-WM
KATIKA kuelekea Sikukuu ya Pasaka, watumishi wa Wizara ya Madini wameungana pamoja kuwatembelea na kutoa msaada watoto yatima wa Kituo cha Tumaini Jema na Kituo cha Watoto cha Nyumba ya Matumaini vilivyopo jijini Dodoma.


“Kwa niaba ya Watumishi wenzangu wa Wizara ya Madini, naomba niwapongeze watoa huduma wote wa kituo hiki kwa kazi kubwa mnayoifanya, naomba muendelee na moyo huo na Mwenyezi Mungu azidi kuwabarki,” amesema Ntuke.
Kwa upande wake, Msimamizi Mkuu wa Kituo cha Watoto cha Nyumba ya Matumaini, Sista Aurea Kiara amesema, kituo anachokisimamia kinapokea watoto kuanzia miaka mitatu ambao wazazi wao wamefariki kwa ugonjwa wa Ukimwi pamoja na watoto wenye maambukizi ya Virusi vya Ukimwi ambao wametengwa na familia zao.

Naye, Msimamizi Mkuu wa Kituo cha Tumaini Jema Exusuper Liyumba amesema kituo anacho liongoza kina jumla ya watoto 18 ambapo hadi sasa kituo kimepata eneo Msalato ambapo kitajengwa kituo kikubwa chenye uwezo wa kuhudumia watoto zaidi ya 128.
Katika kuungana na jamii Wizara ya Madini imekuwa ikishirikiana na vituo mbalimbali vya kuhudumia jamii kwa lengo la kushikana mkono na kupeana faraja katika maisha.