Waziri Bashungwa atoa taarifa njema kwa wakazi wa Ngorongoro wanaohamia Handeni

NA OR-TAMISEMI

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Mhe. Innocent Bashungwa amesema Serikali imetoa shilingi milioni 500 kuanza ujenzi wa kituo cha afya Msomera katika eneo la mradi wa wakazi wanaotoka katika eneo la Hifadhi ya Ngorongoro na kuhama kwa hiari Wilaya ya Handeni mkoa wa Tanga.
Pia, Serikali imetoa shilingi Milioni 50 kwa ajili ya kupanua na kuboresha huduma za afya katika Zahanati ya Kijiji cha Msomera katika kata ya Misima Wilaya ya Handeni mkoa wa Tanga kinachotoa huduma kwa wananchi wasiopungua 10,000.

Ameyasema hayo leo Aprili 15, 2022 wakati wa ziara ya kutembelea na kukagua huduma za msingi za afya, elimu na miundombinu katika eneo la mradi wa wakazi wanaotoka eneo la Hifadhi ya Ngorongoro ambao wanahama kwa hiari katika Kijiji cha Msomera Wilaya ya Handeni mkoani Tanga.

Bashungwa amesema, tayari Serikali imetoa shilingi milioni 400 kuanza ujenzi wa shule mpya za msingi na sekondari na bweni moja katika Kata ya Misima katika Kiijiji cha Msomera ili wanafunzi wasitembee mwendo mrefu kupata masomo ya elimu ya msingi na sekondari.

Aidha, Bashungwa amesema Serikali itaboresha Shule ya Msomera kwa kuongeza vyumba vya madarasa, matundu ya vyoo na kuongeza walimu kutoka na upungufu uliopo kwa sasa katika shule hiyo.
Bashungwa amesema, Serikali kupitia Ofisi ya Rais-TAMISEMI itaongeza watumishi ambao ni wauguzi, wataalam wa maabara na madawa ili ukarabati unaofanyika katika Zahanati ya Msomera uendane na huduma nzuri zinazoendelea kutolewa hapo.

Vile vile, amemuaguza Mkurugenzi Mtendaji wa TARURA kufanya upembuzi yakinifu wa barabara inayotoka Handeni Mjini hadi Kata ya Misima ili iweze kutengewa bajeti ya kuweka kifusi, kujenga makalvati na boksi kalvati katika maeneo korofi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news