Waziri Tax ateta na wanajeshi wastaafu

NA DIRAMAKINI

WAZIRI wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mheshimiwa Dkt. Stergomena Lawrence Tax (Mb) amekutana na kuongea na Wanajeshi wastaafu kutoka jimbo la Uchaguzi la Kawe jijini Dar es Salaam, kwa lengo la kusikiliza changamoto zinazowakabili na kuangalia namna ya kuzitatua.
Mkutano huo uliratibiwa na Mbunge wa Jimbo hilo, Mheshimiwa Askofu Josephat Mathias Gwajima (Mb) na kuhudhuriwa na wastaafu wa vyeo mbalimbali, waliostaafu kwa tarehe na ujuzi tofauti mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa Jacks (Jacks Hall) uliopo eneo la Africana Kunduchi Jijini Dar Es Salaam.

Akiongea na wastaafu hao Mheshimiwa Waziri alianza kwa kumshukuru Mheshimiwa Askofu Gwajima kwa kufanikisha mkutano wake na Wastaafu kutoka jimboni kwake. Aidha, alimshukuru Mheshimiwa Rais kwa jitihada zake za kuhakikisha watu wake wako vizuri.
Mheshimiwa Dkt. Stergomena alibainisha wazi kuwa umuhimu wa mkutano na wastaafu hao kwani umemuwezesha kukutana, kubadilishana nao mawazo na pia kuangalia mfumo mzuri utakaowawesha wastaafu hao kutoa hoja zao kwa lengo la kutatua changamoto zao.

Aidha, Waziri wa Ulinzi na JKT aliwahakikishia wastaafu hao kuwa Wizara yake na serikali kwa ujumla inawathamini wastaafu na inazifahamu Changamoto zote zinazowakabili na tayari baadhi ya changamoto mchakato wa kuzifanyia kazi umeshaanza na kuwaahidi kuwa Wizara inazichukua changamoto zilizowasilishwa katika mkutano huo amezichukua.
Aidha, Wizara kupitia Makao Makao Mkuu ya Jeshi itajitahidi kuzitatua changamoto hizo.

Kwa upande wake, Mheshimiwa Askofu Gwajima akiongea kwenye Mkutano huo, amemshukuru Mhshimiwa Rais kwa maelekezo yake yanayowataka viongozi katika maeneo yao kuwasiliza wastaafu wote katika maeneo yao. “Namshukuru Mheshimiwa rais kwa maelekezo yake ya kututaka tuwasikiliza, kuwajali na kuwasaidia wastaafu wote katika maeneo ya Majimbo yetu,”amesema.
Mkutano baina ya Mheshimiwa Waziri na Wastaafu ulihudhuriwa pia na Kamishna wa Maendeleo na Utafiti kutoka Wizara ya Ulinzi na JKT, Meja Jenerali Salum Othman, Mkuu wa Tawi la Utumishi Jeshini, Meja Jenerali Paul Simuli, pamoja na baadhi ya Wakuu wa Matawi na Wakurugenzi kutoka Makao Makuu ya Jeshi pamoja na wastaafu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news